Mkuu wa IMF Christine Lagarde.
Shirika la Fedha Duniani IMF limeidhinisha msaada wa dola bilioni kumi na saba kuunusuru uchumi wa Ukraine wakati taifa hilo likijitahidi kurejesha utulivu wa kisiasa na kiuchumi.
Msaada huo ulioahidiwa mnamo mwezi Marchi utategemea mabadiliko makubwa ya kiuchumi, ikiwemo kupanda kwa kiwango cha kodi na bei ya nishati mbali na kupigwa tanji kwa mishahara ya chini.
Zaidi ya dola billioni tatu zitakabidhiwa mara moja serikali ya Ukraine ambayo inakabiliwa na mzozo wa kiuchumi pamoja na kisiasa.
Awali mkutano wa kimataifa uliofanyika mjini London ulikamilika na ahadi ya kuisadia Ukraine kuisaka mali ya mamilioni ya madola inayodaiwa kuibwa na aliyekuwa kiongozi wa taifa hilo Victor Yanukovych pamoja na wandani wake.