TAARIFA za awali kutoka eneo la tukio zinaeleza kuwa Watu zaidi ya 20 wamefariki dunia papo hapo na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya basi la kampuni ya Luhuye lililokuwa likitokea Sirari Mkoani Mara Kwenda Kahama kupata ajali katika eneo la Masanza Kona Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu majira ya katikati ya saa nne na saa tano za asubuhi hii leo.
Taarifa za awali zinaeleza kuwa basi hilo liliacha barabara na kugonga nyumba ambapo lilipinduka na kusababisha vifo hivyo huku idadi kubwa ya abiria wakijeruhiwa vibaya.
Maadhi ya majeruhi walikimbizwa katika hospital ya Wilaya ya Magu na wengine katika Hospital ya Rufaa Bugando huku kukiwa na taarifa na idadi ya watu waliopoteza maisha kuongezeka hadi kufikia jioni hii.
Miongoni mwa abiria waliokuwemo katika basi hilo ambao wamepoteza maisha ni Pamoja na Alex Masatu (Dj Alex da Wolf) ambae alikuwa ni mfanyakazi wa Radio Metro iliyoko Mkoani Mwanza.
Taarifa zaidi tutaendelea kukuwasilishia kadri zitakavyo tufikia.