Na Mwandishi Wetu, Mwananchi
Uturuki kupitia Mamlaka ya Usimamizi na Maendeleo ya Nyumba, iliyopo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu (TOKI), iliwahamisha wakazi zaidi ya 6,500 waliokuwa wakiishi kwenye maeneo ya ujenzi holela na sasa eneo hilo katika Mji wa Ankara limepangwa na kuendelezwa upya na baada ya kukamilika litakuwa na uwezo wa kukaliwa na watu zaidi ya 18,000.
Uturuki. Hatua iliyopigwa na Serikali ya Uturuki katika kupanga upya na kuyaendeleza makazi yaliyokuwa na msongamano mkubwa wa watu, imeonekana kuwaduwaza wabunge wa Tanzania ambao wako kwenye ziara ya mafunzo katika miji ya Ankara na Istanbul.
Uturuki kupitia Mamlaka ya Usimamizi na Maendeleo ya Nyumba, iliyopo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu (TOKI), iliwahamisha wakazi zaidi ya 6,500 waliokuwa wakiishi kwenye maeneo ya ujenzi holela na sasa eneo hilo katika Mji wa Ankara limepangwa na kuendelezwa upya na baada ya kukamilika litakuwa na uwezo wa kukaliwa na watu zaidi ya 18,000.
Ujumbe wa wabunge hao, wengi wakiwa wajumbe wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira unaongozwa na Mbunge wa Kuteuliwa, Zakia Meghji (CCM),huku kwa upande wa Serikali unaongozwa na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Goodlucky Ole Medeye.
Wengine katika ziara hiyo iliyoandaliwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ni wawakilishi kutoka Kamati za Bunge za Bajeti na ile ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, pamoja na viongozi wakuu kutoka Halmashauri ya Wilaya za Arusha na Arumeru pamoja na Jiji la Arusha.
Katika ziara hiyo ya siku sita, imebainika kuwa tatizo linalokwaza uendelezaji wa makazi Tanzania ni gharama kubwa za ujenzi ambazo zinachangiwa na bei kubwa ya ardhi, riba ya mikopo ya benki na kodi ya ongezeko la thamani (VAT) baada ya nyumba kujengwa.
Nchini Uturuki, TOKI hupewa ardhi na Serikali kwa gharama ndogo na nyumba zinazojengwa huuzwa pasipo kuongeza faida wala kutozwa kodi kutokana na Serikali kuwekeza fedha nyingi katika sekta hiyo, huku wale wanaouziwa wakilipa fedha hizo kwa miaka 20 bila kutozwa riba.
Meneja wa Tawi la Uhusiano wa Kimataifa katika Idara ya Mipango miji ya TOKI, Sule Karabey alisema gharama za nyumba kwa ajili ya makazi yanayojengwa kwa ajili ya watu wenye kipato cha kati na cha chini, huuzwa kwa fedha ambazo ni sawa na Sh19.2 milioni za Tanzania.
Kiasi hicho ni zaidi ya mara mbili ya gharama za nyumba za bei nafuu zinazojengwa na NHC na kuuzwa kwa wananchi.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemiah Mchechu mara kadhaa amenukuliwa akilalamikia gharama kubwa ya ardhi, kodi kwenye vifaa vya ujenzi na kwenye mauzo ya nyumba kuwa ni kikwazo kwa shirika hilo kujenga nyumba za gharama nafuu.
Juzi, Mchechu aliwaambia wabunge hao kuwa, kikwazo kingine ni kutokuwapo kwa huduma za jamii kama maji, umeme na barabara katika maeneo ambayo shirika lake linayaendeleza na kwamba wakati mwingine NHC hugharimia huduma hizo hivyo kusababisha gharama za nyumba kuongezeka.
Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (Chadema), alisema tatizo lililopo ni kukosekana kwa mawasiliano na uratibu miongoni mwa taasisi za Serikali na kwamba kama yangekuwapo hilo lisingekuwa tatizo.w.hakileo.blogspot.com
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago