MBUNGE MSIGWA AKUTANA NA WAFANYABIASHARA MJINI IRINGA

Mkazi wa Frelimo 'C' katika Manispaaya Iringa, mkoani Iringa, Chagu Maiko Chali akitoa kero yake Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Simon Msigwa ya kutapakaa kwa taka ngumu kila kona ya mjini bila kuzolewa wakati wa mkutano wa wafanyabiashara na mbunge katika Ukumbi wa Olofea leo.



Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Simon Msigwa (Chadema) akitoa ufafanuzi kuhusiana na kero zilizoletwa na wafanyabiashara wakati wa mkutano wa wafanyabiashara na wadau mbalimbali wa maendeleo katika Ukumbi wa Olofea leo.



Katibu wa umoja wafanyabiashara manispaa ya iringa, Jackson Kalole (kulia) akisoma risala kwa niaba ya umoja huo kwa Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Simon Msigwa (Chadema) wakati wa mkutano wa wafanyabiashara na wadau mbalimbali wa maendeleo katika Ukumbi wa Olofea leo.





Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Simon Msigwa (wa pili kulia) akiptia risala ya umoja wa wafanyabiashara wa Manispaa ya Iringa wakati wa mkutano wa wafanyabiashara na wadau mbalimbali wa maendeleo katika Ukumbi wa Olofea leo.



Mhasibu Mapato wa Manispaa ya Iringa, mkoani Iringa, Gloria Karlo (kushoto) akifafanua jambo kwa wafanyabiashara katika Ukumbi wa Olofea leo. Kushoto kwake ni Afisa Biasharawa Manispaa, Mwanasheria wa Manispaa ya Iringa, Catherine Charwe, Mwenyekiti wa umoja wa wafanyabiashara manispaa ya iringa, Odila Ngamilaga na Mbunge wa Iringa mjini, Mch. Peter Msigwa wakati mkutano leo.



Sehemu ya wafanyabiashara mbalimbali wakiwa katika Ukumbi wa Olofea leo.

Mwanasheria wa Manispaa ya Iringa, Catherine Charwe akifafanua masuala ya kisheria kwa wa wafanyabiashara Manispaa ya Iringa leo.


Mwenyekiti wa Umoja wa wafanyabiashara Manispaa ya Iringa, Odila Ngamilaga akifunga mkutano katika Mbunge wa Iringa mjini Mch. Peter Msigwa na wafanyabiashara leo.


Mmoja wa wadau wa maendeleo Manispaa ya Iringa, Mzee David Butinini akitoa kero yake kuhusu manispaa kutokuwa na akaunti ya benki kwa ajili ya wafanyabiashara hao waweze kulipa kodi zao kupitia benki, ili kupunguza urasmi na mianya ya rushwa hatimaye kuongeza ufansi katika utendaji kwa watumishi.



Mkazi wa Iringa mjini, Nicolaus Pinjili akichangia hoja.

Sehemu ya risala iliyosomwa na katibu wa Umoja wa wafanyabiashara, Jackson Kalole kwa mgeni rasmi





Mfanyabiashara Zain Yusuf mkazi wa Miyomboni akichangia hoja.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company