Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji(Ewura)
Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) imefuta leseni za kufanya biashara ya mafuta kwa jumla (Whole Sale Licenses) kwa Kampuni tisa zinazojihusisha na biashara hiyo hapa nchini.
Uamzi huo umefanywa jana katika kikao chache cha Bodi ya Wakurugenzi kilichoongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Ewura, Simon Sayore, kutokana na kampuni hizo kukiuka masharti ya biashara.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Felix Ngamlagosi, kufutwa kwa leseni hizo kumetokana na ukikaji kwa sheria na kanuni za biashara hiyo.
Ngamlagosi katika taarifa yake, alisema kampuni hizo zimefutiwa leseni kutokana na kukaa bila kuagiza mafuta kama leseni inavyowataka kwa kipindi cha zaidi ya miezi sita tangu kupewa leseni hizo na Ewura.
Kampuni zilizofutiwa leseni ni pamoja na Aspam Energy (T) Limited, MPS Oil Tanzania Limited, Panone Bulk Oil Importers Limited, Petcom (T) Limited, KMJ Tanzania Limited, Horizon Petroleum Company Limited, G.M and Company (T) Limited na Petronas Energy Tanzania Limited.
CHANZO: NIPASHE
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago