Kampuni ya Global Publishers & General Enterprises Ltd, wachapishaji wa Magazeti ya Uwazi, Championi, Amani, Risasi, Ijumaa na Ijumaa Wikienda jana ilizindua Global TV Online ambayo ni televisheni inayoruka mtandaoni kupitia tovuti ya kampuni hiyo ya www.globalpublishers.info ndani ya ofisi zake zilizopo Mwenge-Bamaga jijini Dar es Salaam. Katika uzinduzi huo, mastaa kibao walihudhuria na kupata fursa ya kuona baadhi ya vipindi kutoka Global TV Online pamoja na kutoa maoni yao kuhusu uboreshwaji wa TV hiyo. Mbali na tukio hilo, mastaa waliongoza zoezi la kukata utepe, kufungua shampeini na kukata keki kuashiria uzinduzi rasmi wa Global TV Online.
Kutoka kushoto: Wasanii Dk. Cheni, Bi. Mwenda, Profesa Jay na Wema Sepetu wakishiriki kukata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa GlobaL TV Online jana.
GlobaL TV Online baada ya kuzinduliwa rasmi.
Mkongwe wa sanaa ya maigizo Bongo, Fatuma Makongoro 'Bi. Mwenda' akijiandaa kufungua shampeini.(A.I)
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago