WATU WATATU WAKAMATWA NA BHAGI KILO 133.5 MKOANI DODOMA.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma David A. Misime - SACP akiongea na wanahabari
Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma linawashikilia watu watatu kwa kosa la Kupatikana na Bhangi kiasi cha Kilogramu 133.5 yenye thamani ya Ths. 20,025,000/= bei ya mitaani (street value). Watuhumiwa hao wamekamatwa mnamo tarehe 16/04/2014 majira ya 7:30 mchana eneo la Stend Kuu ya mabasi katika Manispaa na Mkoa wa Dodoma. Watuhumiwa hao walikuwa wakisafirisha Bhangi katika mabegi baada ya kupanda basi kutokea Kijiji cha MANONGA – TINDE Mkoani SHINYANGA kwenda jijini Dar es Salaam katika basi namba No. T.931 CGU mali ya kampuni ya NEW FORCE linalofanya safari zake kutokea Kahama kwenda jijini Dar es Salaam. Watu hao walifahamika kwa majina ya:-

1. CALVIN S/OPROSPER SALEKA, miaka 23, kabila Mchaga, Mwanafunzi wa chuo cha Institute of Finance Management (IFM) cha Dar es Salaam, mwaka wa pili, alikamatwa akiwa na mabegi mawili ya bhangi yenye uzito 51kgs

2. JOHN S/O JOSEPH,

Miaka 31, kabila msukuma, mkulima na mkazi wa Kinondoni Dar es Salaam,
alikamatwa akiwa na mabegi mawili ya bhangi yenye uzito wa 42.5kgs.
3. JOSEPH S/O

CHARLES BATONI, Miaka 22, kabila msukuma, mkulima na mkazi wa Shinyanga.
alikamatwa akiwa na mabegi mawili ya bhangi yenye uzito 36.5kgs

Watuhumiwa hao walikamatwa kufuatia taarifa za raia mwema aliyewatilia mashaka na kutoa taarifa Polisi. Mbinu waliyotumia kusafirisha ni kuhifadhi katika mabegi makubwa ya nguo na kufunga kwa mifuko ya nailoni kisha kusaga vitunguu na kuweka katika mabegi hayo pamoja na kupulizia manukato (perfume) ili kuondoa harufu wasiweze kugundulika kirahisi.

Tukio lingine katika kijiji cha Central Kiteto Tarafa ya Mlali Wilaya ya Kongwa zilikamatwa lita 300 za Pombe haramu ya Gongo nyumani kwa Salumu s/o Chamagulu ambaye alikimbia baada ya kuona Polisi na tunaendelea kumtafuta.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi David A. Misime – SACP, anawapongeza kwa dhati raia wema wanaoshirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ili kuendelea kudhibiti madawa ya kulevya na Pombe ya Moshi inayoharibu vijana wengi.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company