ZIUWE SABABU KWA NINI RONALDO NI BORA DUNIA NZIMA, KULIKO MESSI NA WENGINEO

NYOTA Cristiano Ronaldo amempoteza Lionel Messi kwa mara nyingine tena, baada ya usiku wa jana kuvunja rekodi ya mabao ya Muargentina huyo, na kuibuka mchezaji aliyefunga mabao mengi zaidi kwa msimu mmoja wa Ligi ya mabingwa Ulaya.
Mkali huyo wa Ureno jana alifunga mabao mawili katika ushindi wa wa Real wa 4-0 kwenye mchezo wa marudiano wa Nusu Fainali dhidi ya Bayern Munich, na kufikisha jumla ya mabao 16 kwa msimu huu.

Mvunja rekodi: Cristiano Ronaldo ndiye mchezaji aliyefunga mabao mengi zaidi kwa msimu mmoja katika Ligi ya Mabingwa Ulaua (16)

Rekodi hiyo ya Ronaldo inaipiku rekodi ya Lionel Messi - ambaye alifunga mabao 14 kwa Barcelona msimu wa 2011-12.
Tangu ahamie Madrid mwaka 2009, mshambuliaji huyo amefunga jumla ya mabao 250 katika mechi 243 za klabu hiyo.

Ronaldo alifunga bao la tatu na la nne Real jana katika ushindi huo Uwanja wa Allianz Arena kuvunja rekodi hiyo baada ya mashambulizi nya kushitukiza.


Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Ureno mwenye umri wa miaka 29, kufunga mabao mawili haikuwa rekodi pekee jana aliyoweka mjini Munich.
Mabao mawili ya mshindi huyo wa tuzo ya Ballon d'Or pia yanamfanya awe mchezaji wa tatu katika historia ya mashindano hayo kufikisha mabao 50 au zaidi aliyoifungia timu moja katika Ligi ya Mabingwa.
Ronaldo aliyefunga mabao 51 katika mechi 50, anamfuataia gwiji wa Real, Raul aliyefunga mabao 66 na Messi wa Barcelona mwenye mabao 67.

MABAO 16 YA RONALDO MSIMU HUU
Mabao mawili ya Cristiano Ronaldo aliyoifungia Real Madrid dhidi ya Bayern Munich wa jana yanamfanya atimize mabao 16 msimu huu katika Ligi ya Mabingwa.
Anakuwa mchezaji aliyefunga mabao mengi zaidi kwa msimu mmoja wa Ligi ya Mabingwa Ulaya...
Galatasaray 1-6 Real Madrid, Septemba 17, 2013 - Ronaldo mabao matatu (3)


Real Madrid 4-0 Copenhagen, Oktoba 2, 2013 - Ronaldo mabao mawili (2)
Real Madrid 2-1 Juventus, Oktoba 23, 2013 - Ronaldo mabao mawili (2)

Juventus 2-2 Real Madrid, Novemba 5, 2013 - Ronaldo bao moja (1)

Copenhagen 0-2 Real Madrid, Desemba 10, 2013 - Ronaldo bao moja (1)





Schalke 1-6 Real Madrid, Februari 26, 2014 - Ronaldo mabao mawili (2)




Real Madrid 3-1 Schalke, Machi 23, 2014 - Ronaldo mabao mawili (2)




Real Madrid 3-0 Borussia Dortmund, Aprili 2, 2014 - Ronaldo bao moja (1)




Bayern Munich 0-4 Real Madrid, Aprili 29, 2014 - Ronaldo mabao mawili (2)

CHANZP BIN  ZUBEIRY
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company