Na Prince Akbar, Dar es Salaam
AZAM FC imewaacha wachezaji saba katika kikosi kilichomaliza na ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu huu, wakiwemo viungo Jabir Aziz na Ibrahim Mwaipopo.
BIN ZUBEIRY inafahamu Aziz na Mwaipopo wamemaliza mikataba yao na Azam FC, ambayo imekwishawaambia haitawaongezea mikataba, wakati mabeki Samih Haju Nuhu na Luckson Kakolaki wanastaafu kwa sababu mbalimbali.
Jabir Aziz ni kati ya wachezaji saba waliotemwa Azam FC
Nuhu ameumia goti ambalo hana matumaini ya kupona karibuni, wakati Kakolaki ameamua mwenyewe kustaafu na ataingizwa katika benchi la Ufundi la akademi ya klabu.
Aidha, mshambuliaji kutoka Ivory Coast, Ismail Kone anamaliza Mkataba wake Novemba mwaka huu, lakini amefikia makubaliano na klabu kuuvunja, wakati Malika Ndeule na Omar Mtaki wanaungana na Aziz na Mwaipopo ambao wamemaliza mikataba na hawaongezwi.
Tayari Azam FC imesajili wachezaji wapya watatu, ambao ni washambuliaji Didier Kavumbangu wa Burundi, Ismaila Diarra kutoka Mali na mzalendo Frank Domayo.
Usajili wa Kavumbangu na Diarra unafanya Azam iwe na wachezaji watano wa kigeni, wengine wakiwa ni Kipre Herman Tchetche na Kipre Michael Balou, ndugu wawili na pacha kutoka Ivory Coast Mganda Brian Umony.
Mabingwa hao wapya wa Bara, wanatarajiwa kuboresha zaidi kikosi ili msimu ujao waweze kushiriki vyema Ligi ya Mabingwa Afrika na kutetea ubingwa wa nchi.
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago