Majaji wakiwa kazini katika Shindano lililofanyika Kanda ya Ziwa Mkoani Mwanza
Jaji Mkuu wa Shindano la Tanzania Movie Talents, Roy Sarungi akiwa Kazini
Jaji Wa Pili, Vyonne Chery "Monalisa"
Jaji wa Tatu, Single Mtambalike "Rich Rich"
Shindano la Tanzania Movie Talents ni shindano lililoanzishwa na Kampuni ya PROIN PROMOTIONS LIMITED ambapo kwa mara ya kwanza limepata kufanyika Nchini Tanzania na Afrika Mashariki na Kati.
Kama ilivyo kawaida kwenya mashindano yoyote yale lazima washindi wapatikane na watambulike na kuna baadhi ya mashindano ambapo washindi hupatikana kwa kuchaguliwa na majaji katika awamu zote za shindano husika na baadae Majaji hao kuweza kumchagua mshindi au washindi kutoka na Sifa, Vigezo na Masharti ya Shindano hilo.
Shindano la Tanzania Movie Talents ni shindano mojawapo ambalo limepewa baraka zote na Serikali kupitia taasisi yake ya BASATA na kutokana na kupewa vibali sehemu kusika maana yake kuwa shindano hili liliweza kukidhi vigezo na masharti vilivyotolewa na BASATA.
Na shindano hili ni shindano linaloendeshwa kwa taratibu na sheria ambazo kampuni ya PROIN PROMOTIONS Imeziweka kwa kushirikiana na BASATA ili kuhakikisha shindano hili linakuwa ni la wazi, haki na usawa bila kupendelea mtu au majaji kuwachagua washindi kwa hisia zao binafsi.
Na Ubora wa Shindano hili umeanza kudhihirika pale Ambapo majaji waliweza kufuata taratibu, sheria, vigezo na masharti ya shindano hilo na hatimaye kupata washindi wanaostahili. Majaji wa shindano hili hawaangalii uzuri wa Sura ya Mtu, Hawaangalia huyu ni nani au nani wanachoangalia ni kufuata vigezo na masharti ya shindano hilo na sifa za mshiriki. Majaji wa shindano hili la Tanzania Movie Talents Wamedhirisha uwezo wao kuwa wanafanya kazi kwa kufuata taratibu na sheria za shindano hili la Tanzania Movie Talents.
Majaji wa Shindano hili ni Kama Ifuatavyo Jaji Mkuu ni Roy Sarungi akisaidiwa na Single Mtambalike "Rich Rich" na Vyonne Chery "Monalisa" hawa ndio majaji walioweza kufanikisha shindano hili kwa hatua hii ya Kwanza kwa Kanda tatu ambazo tayari washindi wameshapatikana. Ni Imani yetu kuwa wataendelea na moyo huohuo wa kufuata taratibu na sheria ilikuweza kutenda haki katika shindano hilo linalotarajiwa kuendelea kufanyika katika Kanda ya Kusini Mkoani Mtwara tarehe 7 May 2013 na kanda nyingine zilizobakia.
CHANZO LUKAZA