Ban Ki-moon ziarani Sudani Kusini


Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, akiwasili katika mji mkuu wa Sudani Kusini, Juba.
REUTERS/Jonny Hogg Na RFI

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon amewasili mapema leo asubuhi nchini Sudani Kusini kwa ziara ya kikazi ya siku moja, ili kujaribu kushawishi pande zote husika katika mgogoro unaoendelea kuwajibika na ujenzi wa taifa hilo.
Ziara hii ya Ban inakuja baada ya ziara ya waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani Jonh Kerry hapo ijumaa, kujaribu kuzikutanisha pande mbili husika katika mchakato wa amani. Umoja wa Mataifa na Marekani walitahadharisha dhidi ya kutokea kwa mauaji ya kimbari nchini Sudani Kusini.

Mapigano yanaendelea licha ya makubaliano ya kusitisha vita yaliyosainiwa januari 13 mjini Addis Ababa, licha ya vitisho vilivyotolewa na Marekani. Mazungumzo ya kusaka amani mjini Addis Ababa yanasuasua.

Tangu mapigano yalipozuka, Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon amekua akitolea wito pande husika kutafuta suluhu la kisiasa na kukomesha machafuko ambayo yamesababisha maelfu ya raia kupoteza maisha na maelfu wengine kuhama makaazi yao, ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Sudani Kusini, imefahamisha.

Kwa mujibu wa ofisi hio ya Umoja wa Mataifa nchini Sudani Kusini (UNMIS), Ban atakutana kwa mazungumzo na rais wa Salva Kiir, na atatembelea moja kati ya maeneo ya Umoja wa Mataifa linalowapa hifadhi wakimbizi takriban 800.000 wa Sudani kusini, ambao waliyakimbia mapigano, huku wakiishi katika mazingira magumu.

Kambi iliyoko kwenye moja ya maeneo ya Umoja wa Matiafa karibu na uwanja wa ndege wa Juba ikiwahifadhi watu 12.000 wa jamii ya Nuer waliyokimbia mapigano, Decemba 24 mawaka 2013.Reuters/

Mapigano makali yameendelea leo jumapili, kando na Bentiu, mji mkuu wa jimbo lenye utajiri wa mafuta wa Unity (kaskazini mashariki mwa Sudani Kusini).

Jeshi linalomuunga mkono rais Kii linajaribu tangu jumapili kurejesha kwenye himaya yake mji huo wa Bentiu, ambao ulitekwa hivi karibuni na waasi wanaomuunga mkono Riek Machar, ambae alianzisha vita dhidi ya serikali ya rais Salva Kiir tangu desemba 15 mwaka 2013.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company