Marekani imewapa waasi wa Misri hadhi ya kidiplomasia ambapo wamefungua afisi nchini humo.
Hatua hiyo ilitangazwa wakati wajumbe wa muungano wa waasi walipowasili mjini Washington katika ziara yao rasmi ya kwanza nchini humo.
Hata hivyo Marekani haitambui muungano wa waasi hao wa Syria kama Serikali ya taifa lao na wala hawaruhusiwi kuingia katika ubalozi wa Syria.
Maafisa wa Serikali ya Marekani walisema hatua hiyo imechukuliwa kama hatua ya kujaribu kuimarisha uhusiano na upande wa upinzani wenye msimamo wa kadiri.
Hatua hii itasaidia huduma za benki na usalama, na wakati huohuo kusaidia makundi ya upinzani kuimarisha sifa ya Marekani miongoni mwa raia wa Syria wanaoishi ng'ambo.
Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Marekani imetangaza msaada zaidi wa Dola milioni 27 kwa muungano huo wa waasi.
Hadi kufikia sasa Marekani imeendelea kutoa misaada isiyo ya silaha ingawa baadhi ya maafisa Serikalini wamependekeza kuwa msaada wa kijeshi uanze kutolewa kwa waasi hao.
CHANZO BBC SWAHILI