Fatou Bensouda |
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mjini New York, Bi Bensouda amesema, ofisi yake ilipeleka malalamishi kwa majaji wa ICC kuhusu ukosefu wa ushirikiano wa Kenya kuhusu kesi hiyo, ambayo iliakhirishwa hadi Oktoba mwaka huu.
Mwanasheria huyo wa ICC amesema ingawa kesi dhidi ya makamu wa rais, William Ruto, inaendelea, bado inakumbana na vikwazo vingi. Bensouda amesema tatizo kubwa ni mashahidi wa upande wa mashtaka ambao ama hawataki kujitokeza, au wanabadili mawazo yao dakika ya mwisho.
Umoja wa Afrika umeikosoa vikali ICC na kusema ni mahakama yenye malengo ya ukoloni mamboleo kwani inawalenga tu viongozi wa Afrika na kupuuza jinai katika maeneo mengine ya dunia. AU imesema viongozi walioko madarakani hawapaswi kufikishwa katika mahakama hiyo yenye makao yake The Hague Uholanzi.
CHANZO RADIO IRAN SWAHILI