Malkia Mpya wa Kijiji cha Maisha Plus Elizabeth Masha kutoka Morogoro Tanzania
Ndani ya Kijiji cha Maisha Plus/ Mama Shujaa wa chakula kila siku ya Alhamisi huwa panafanyika uchaguzi wa kumpata Rais mpya ambaye anachaguliwa na Washiriki wenyewe wa Kijiji cha Maisha Plus ambapo kati ya hao mmoja hupatikana na Marais waliopita hawapatiwi nafasi ya kugombea tena, na kwamba mama yake na Rais huteuliwa moja kwa moja kuwa Malkia wa Kijiji hicho.
Rais Mpya wa Kijiji cha Maisha Plus Mary Masha kutoka Nchini Kenya
Kazi ya uchaguzi ilianza Kijijini hapo ambapo idadi ya washiriki 36 wakiwemo vijana 16 na kinamama 20 Kila siku ya Alhamisi ni siku ya uchaguzi wa Rais wa kijiji cha Maisha Plus ambaye husimamia shughuli zote zinazofanyika katika kijji hicho.
Wiki hii washiriki 10 waliteuliwa kugombea nafasi ya urais ambapo 7 ndiyo waliopigiwa kura ya siri na kupata mshindi. Washiriki wawili kati yao hawakuweza kugombea nafasi ya hiyo kutokana na utaratibu uliopo kwamba aliyewahi kushika wadhifa huo kwa muhula uliopita hataweza kugombea tena.
Marais hao wa mihula uliyopita ni Bonifas Mang’anyi na Bakari Khalid wote watanzania. Abdul Karim kutoka Burundi alijitoa kwa kuwa hakuwa tayari kushika wadhifa huo kwa sasa.
Kwa kawaida kila kijana huwa na mama katika kijiji cha Maisha Plus na endapo kijana atachaguliwa kuwa Rais mama yake huwa Malkia ambaye humshauri Rais na kufanya maamuzi katika kijiji hicho.
Uchaguzi ulifanyika kwa wagombea 7 akiwemo Shida Mganga, Seif Mohamed, Ally Thabiti, Mbonimpaye Nkoronko na Hyasinta Hokororo kutoka Tanzania, Ngabozinza Daniel kutoka Rwanda na Mary Masha kutoka Kenya. Uchaguzi wa Rais ulifanyika mara mbili kwa kuwa washindi walipata kura sawa iliyopelekea kurudia kupiga kura ili kupata mshindi mmoja.
Washindi waliopata kura sawa ni Mary Masha kutoka Kenya na Ally Thabit kutoka Tanzania ambapo Mary Masha aliibuka mshindi kwa kura 21 kwa 15. Hivyo Rais wa wiki hii ni Mary Masha na malkia Elizabeth Simon.
Utaratibu wa kuchagua wagombea: Kila mshiriki hujaza fomu kuteua jina la atakayekuwa kuwa Rais wa wiki hiyo. Walioteuliwa hujinadi ili wapate kupigiwa kura na hatimaye kupata mshindi.