Watu 15 wauliwa Jamhuri ya Afrika ya Kati


Watu 15 wameuawa katika shambulio lililofanywa na watu wenye silaha wasiofahamika huko mashariki mwa kitongoji cha Markanda umbali wa kilomita 30 kutoka katika mpaka wa Jamhuri ya Afrika ya Kati na Chad. Maafisa wa kieneo wa wafanyakazi wa taasisi za misaada ya kibinadamu za nchi za nje zinazotoa huduma huko Jamhuri ya Afrika ya Kati wamesema kuwa shambulizo hilo limetekelezwa na wanamgambo wa Kikristo wa Anti Balaka. Wameeleza kuwa, raia wengine kadhaa wamejeruhiwa katika shambulizi hilo lililofanywa na wanamgambo wa Anti Balaka huko Markanda.

Wakazi wengi wa kitongoji cha Markanda wamekimbia makazi yao na kwenda kutafuta hifadhi katika vijiji vya karibu baada ya kutokea shambulio hilo. Itakumbukwa kuwa, watu wengine wasiopungua 16 waliuawa katika shambulizi lililofanywa siku kadhaa zilizopita na watu wenye silaha wasiofahamika dhidi ya kituo kimoja cha Jumuiya ya Madaktari Wasio na Mipaka, karibu na mpaka kwa Jamhuri ya Afrika ya Kati na Chad.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company