|
Dkt. Karanja Kibicho |
Serikali ya Kenya imesema leo kuwa baadhi ya nchi za Magharibi si marafiki wa kweli na kwamba mienendo yao imechangia kushika kasi uhusiano wa Nairobi na nchi za Mashariki. Tamko hilo lililotolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Dkt. Karanja Kibicho, ni radiamali kwa hatua ya Ufaransa, Uingereza, Marekani na Australia ya kuwataka raia wao wasiitembelee Kenya kutokana na kile kinachodaiwa ni uwezekano wa kutokea mashambulizi ya kigaidi. Kibicho amesema nchi hizo badala ya kuisaidia serikali ya Nairobi kupambana na ugaidi, zimeamua kuchukua hatua za kudhoofisha sekta ya utalii ya nchi hiyo ya Afrika Mashariki. Amewataka Wamagharibi kuiga mfano wa nchi za Mashariki hususan China ambayo miamala yake na nchi za Kiafrika ni ya kidugu na yenye maslahi ya pande zote husika.
CHANZO IRAN RADIO SWAHILI