Kenya yasema haitaondoa majeshi nchini Somalia

Naibu Rais wa Kenya, William Ruto, amesema kuwa serikali ya nchi hiyo haitoondoa majeshi yake katika nchi jirani ya Somalia licha ya kushtadi hujuma za kigaidi za kundi la al-shabab dhidi ya raia wasio na hatia katika miji mbalimbali ya Kenya. Ruto amesema serikali haitokubali kutishwa au kupigishwa magoti na magaidi na kwamba jeshi la nchi hiyo litaendelea kukabiliana na wanamgambo wa al-Shabab ndani ya Somalia hadi pale nchi hiyo itakapopata serikali madhubuti. Naibu Rais wa Kenya amesema kuondoa jeshi nchini Somalia kutatoa fursa kwa al-shabab kujiimarisha upya na kuvuruga amani sio tu ndani ya Somalia bali pia katika nchi zingine za Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika kwa ujumla.

Kambi ya upinzani nchini Kenya imetoa wito kwa serikali kuondoa majeshi nchini Somalia kwa madai kwamba mashambulizi ya al-sahabab dhidi ya raia wa Kenya yanatokana na kuendelea kuweko majeshi ya KDF katika ardhi ya Somalia.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company