Machar akubali kukutana ana kwa ana na Rais Kiir

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki moon, amesema kuwa kiongozi wa waasi nchini Sudan Kusini, Riek Machar, amekubali kukutana ana kwa ana na Rais Salva Kiir ili kutatua mgogoro unaoendelea kuikaba koo nchi hiyo changa zaidi barani Afrika. Ban Ki moon amesema hayo baada ya kufanya ziara ya siku moja huko Sudan Kusini hapo jana. Katibu Mkuu wa UN ameongeza kuwa, Rais Salva Kiir pia amemuhakikishia kwamba yuko tayari kufanya mazungumzo ya moja kwa moja na hasimu wake, Riek Machar mjini Addis Ababa, Ethiopia. Ziara ya mkuu huyo wa UN nchini Sudan Kusini imefanyika huku wanajeshi wa serikali na waasi wakiendelea kupigania udhibiti wa mji muhimu wa Bentiu wenye utajiri mkubwa wa mafuta. Sudan Kusini ilitumbukia katika vita na machafuko ya ndani Disemba 15 mwaka jana baada ya Rais Salva Kiir kumtuhumu makamu wake wa zamani, Riek Machar kuwa alifanya jaribio la kupindua serikali yake.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company