Na Renatus Mahima, Mbeya
NYOTA wawili wa Yanga SC, beki Kevin Yondani na mshambuliaji Mrisho Ngassa wamerejeshwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kinachojiandaa kwa mechi ya hatua ya kwanza kuwania kufuzu kushiriki fainali zijazo za Mataifa ya Afrika (AFCON) dhidi ya Zimbabwe itakayopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kati ya Mei 16 na 18 mwaka huu.
BIN ZUBEIRY ilimshuhudia Yondani aliyekuwa amevaa suti za michezo akiwa jukwaani na baadhi ya wachezaji wa Stars ambao hawakuwamo kwenye orodha ya nyota 20 ya kocha mpya Mholanzi Mart Nooij kwa ajili ya mechi yao ya kimataifa ya kirafiki waliyotoka suluhu na timu ya taifa ya Malawi (The Flames) kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijinin hapa.
Mrisho Ngassa anarejea kikosini Stars baada ya kupona
Aidha, Ngassa ameiambia BIN ZUBEIRY jana kwamba ametumiwa tiketi akiwa kwao Mwanza ambako alikwenda kwa matibabu na jana hiyo hiyo alipanda ndege kwenda Dar es Salaam kuunganisha ndege ya kwenda Mbeya.
Ngassa aliuamia mazoezini wiki mbili zilizopita wakati Stars inajiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Burundi na sasa baada ya kupona yuko tayari kwa majukumu ya kitaifa.
Yondani, mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) msimu wa 2012/13, aliondolewa kwenye kikosi cha Stars Aprili 27 kwa kile kilichotajwa kuwa utovu wa nidhamu kwa kutoripoti kwa wakati mwafaka katika kambi ya timu hiyo jijini hapa.
Walipotafutwa na BIN ZUBEIRY jijini hapa jana kuzungumzia suala hilo, Meneja wa Taifa Stars, Boniface Clement na Kocha Msaidizi, Salum Mayanga hawakupokea simu huku Ofisa Habari na Mawasiliano wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Boniface Wambura akieleza kuwa hajaambiwa chochote juu ya kurejeshwa kwa nyota huyo wa Yanga.
Lakini mmoja wa wachezaji wa Stars aliiambia BIN ZUBEIRY jijini hapa jana kuwa Yondani alirejeshwa juzi kambini mjini Tukuyu.
Taifa Stars inatarajiwa kurejea jijini Dar es Salaam Alhamisi, lakini Wambura aliidokeza BIN ZUBEIRY jijini hapa jana kuwa huenda timu hiyo ikaongezwa muda zaidi wa kambi mjini Tukuyu jijini hapa kutokana na sababu ambazo hakuziweka wazi hata hivyo.
#USOPEN_VIGOGO CHALI
-
SIKU Safi kwa Muaustralia Nick Kyrgios baada ya ushindi dhidi Johnson na
kutinga raundi ya Pili.
- Rafael Nadal akimchapa Millman Seti Tatu zote mfululi...
5 years ago