WACHEZAJI wa Liverpool, akiwemo Luis Suarez usiku wa kuamkia leo walimwaga machozi uwanjani baada mechi ya Ligi Kuu ya England dhidi ya Crystal Palace iliyomalizika kwa sare ya kufungana mabao 3-3 ugenini.
Hadi dakika ya 79, Liverpool walikuwa mbele kwa mabao matatu dhidi ya Crystal Palace, pointi tatu zaidi ya Manchester City katika mbio za ubingwa na kupunguza wastani wa mabao wanayozidiwa hadi kubaki sita.
Lakini upepo ulibadilika na wakaambulia sare, hivyo sasa wanaizidi pointi moja City wakiwa pia wamecheza mechi moja zaidi- maana yake ndoto za ubingwa zimeanza kuyeyuka.
Hawezi hata kutazama: Tegemeo la mabao la Wekundu wa Anfield, Luis Suarez akisikitika baada ya mechi waliyoongoza kwa mabao 3-0 kwa zaidi ya robo tatu ya mchezo, lakini wakamaliza kwa sare ya 3-3
Ganzi: Nahodha wa Liverpool, Steven Gerrard akiwa haamini macho yake baada ya mechi na chini ni mshambuliaji Daniel Sturridge akiugulia maumivu pia ya matokeo hayo
Liverpool ilipata mabao yake kupitia kwa Allen dakika ya 18, Sturridge dakika ya 53 na Suarez dakika ya 55, kabla ya Palace kuzinduka na kuchomoa haraka haraka kupitia kwa Delaney dakika ya 79, Gayle dakika ya 81 na 88.
Hakika ilikuwa huzuni kwa wachezaji wa Liverpool baada ya kushindwa kuondoka na pointi zote tatu- maana yake sasa wana kazi ya kuhakikisha wanashinda mechi zao zote zilizobaki, huku wakiwoambea dua mbaya wapinzani wao, Man City.
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago