Waandamanaji wakipambana na polisi Uturuki siku ya Wafanyakazi
aandamano na vurugu zimefanyika leo siku ya siku ya wafanyakazi duniani katika mji mkuu wa Uturuki wa Istanbul na maeneo mengine duniani.
Maafisa wa polisi walitumia mabomu ya kutoa machozi pamoja na maji baada ya waandamanaji kukaidi marufuku ya kuandamana katika bustani Taksim.
Mamia ya watu kwa makundi walikuwa wakiandamana katika maeneo mbali mbali ya mji huo Shirika la Habari la Associate Press limesema. Wengi wameapa kukaidi amri ya kuwazuia.
Wandamanaji wakiwatupia polisi fataki
Waandamanaji wakijikinga na vifaa vya kuzuia madhara ya mabomu ya machozi
Medani ya Taksim Square
Vyombo vya habari vya nchi hiyo vimewaonyesha waaandamanaji waliobeba bendera wakiwakabili ukuta uliowekwa na polisi wapatao 400 wa kutuliza ghasia.
Serikali ya Uturuki imewapeleka mamia ya maelfu ya maafisawa polisi pamoja na kusimamisha usafiri wa umma.
Waziri Mkuu Recep Tayyip Erdogan mapema aliwaonya watu walikuwa na matumaini ya kukusanyika kwenye medani ya Taksim kuwa itaonyesha ni hatua ya kuipinga serikali.
Nako nchini Cambodia ,watu kadhaa wamedaiwa kupigwa na polisi wanaolinda usalama walipojaribu kuvuruga maandamano ya wapinzani waliokuwa wakiandamana katika mji mkuu wa Phnom Penh.