
Mwakilishi wa Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara Bw. Salumu Masalanga (katikati) akipokea msaada wa pedi kwa niaba ya wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Maendeleo chini ya programu ya Hakuna Wasichoweza iliyofadhiliwa na Vodacom na T-MARC. Wakishuhudia tukio hilo, ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Jamii Vodacom, Yesaya Mwakifulefule (kushoto) na Mratibu wa Mradi kutoka T-MARC Tanzania, Bi. Dorice Chalambo (wa pili kulia), mradi huo umeanza kufanya kazi mkoa wa Mtwara na Lindi na kusambaa nchi nzima.

Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Jamii Vodacom, Yesaya Mwakifulefule (kushoto) na Mratibu wa Mradi kutoka T-MARC Tanzania, Bi. Dorice Chalambo (wa pili kulia) kwa pamoja wakikabidhi msaada wa pedi kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Maendeleo chini ya programu ya Hakuna Wasichoweza iliyofadhiliwa na Vodacom na T-MARC. Akishuhudia tukio hilo (katikati) ni Mwakilishi wa Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara Bw. Salumu Masalanga, mradi huo umeanza kufanya kazi mkoa wa Mtwara na Lindi na kusambaa nchi nzima.
Wasichana wa mkoani Mtwara wamefaidika na elimu ya afya pamoja na vifaa vitakavyowasaidia kujisitiri wakati wa Hethi.