KIKOSI cha Cameroon kilitarajiwa kuondoka jana usiku mjini Younde kuelekea Brazil baada ya kutatuliwa kwa mgogoro wa posho zao.
Waziri Adoum Garoua alisema jana “Kila mmoja yuko tayari kuondoka Saa 3:30 (usiku wa jana) kwenda Brazil. Kila kitu kimefafanuliwa. Hakuna matatizo zaidi,”.
Wachezaji wa Simba Wasiofinguka jana waligoma kupanda ndege kwenda Brazil kwa ajili ya Kombe la Dunia ili kushinikiza malipo ya posho za kushiriki michuano hiyo na kubaki katika hoteli yao mjini Yaounde, wakati Waandishi wa Habari walikuwa nje ya ofisi za Shirikisho la Soka Cameroon kupata maelezo juu ya sakata hilo.
Ndege ilitarajiwa kuondoka Yaounde Saa 3:00 asubuhi ya jana kwenda Brazil, wakati Cameroon inacheza mechi yake ya ufunguzi Ijumaa na Mexico.
Yamekwisha: Wachezaji wa Cameroon walitarajiwa kuondoka usiku wa jana kwenda Brazil
Wachezaji wa Cameroon wiki iliyopita walitaka kugoma hadi kwanza wapewe posh zao, lakini wakasitisha mgomo huo na kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Ujerumani Jumapili iliyopita, liliripotia gazeti la L'Equipe la Ufaransa. Cameroon ipo Kundi A na wenyeji Brazil, Croatia na Mexico.
#USOPEN_VIGOGO CHALI
-
SIKU Safi kwa Muaustralia Nick Kyrgios baada ya ushindi dhidi Johnson na
kutinga raundi ya Pili.
- Rafael Nadal akimchapa Millman Seti Tatu zote mfululi...
5 years ago