NYOTA
Lionel Messi usiku wa jana ameiongoza Argentina kuichapa mabao 3-0
Trinidad and Tobago katika mchezo wa kujiandaa na Kombe la dunia mjini
Monumental.
Mabao
ya Argentina yalifungwa na mshanbuliaji Rodrigo Palacio, kiungo Javier
Mascherano aliyemalizia mpira wa adhabu wa Messi na Maxi Rodriguez.
Palacio,
alicheza badala ya Gonzalo Higuain ambaye anasumbuliwa na misuli,
aliyetoka nje dakika ya 15 baada ya kutonesha kifundo cha mguu.
Baada
ya mechi, Messi alisema: "Wachezaji ambao hawajaingia kwenye kikosi cha
mwisho? Ilikuwa ngumu, Ever (Banega) ni rafiki yang wa karibu, lakini
kocha amefanya maamuzi.
"Tunahitaji kumaliza mchezo vizuri. Kitu cha muhimu ni kuepuka kuumia na kujiweka katika hali ya kujiamini,".
Timu ya Alejandro Sabella itamenyana na Slovenia katika mchezo wao wa mwisho kupasha kabla ya Kombe la dunia.
Argentina, inatazamiwa kutwaa taji lao la tatu la Kombe la Dunia, ikiwa kundi F pamoja na Bosnia, Iran na Nigeria.