KAMA ULIPITWA NA TAARIFA HII NA PICHA ZAKE:ZITTO RASMI ACT, APEWA KADI NAMBA 007194, KUONGEA NA WANAHABARI LEO

Zitto Kabwe akikabidhiwa rasmi kadi ya uanachama wa ACT.
HAYAWI hayawi…Sasa yamekuwa licha ya kusemwa sana kwa muda mrefu juu ya kuhusishwa na chama kipya cha siasa cha ACT-Tanzania dhidi ya aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Ruyagwa Kabwe sasa yamekuwa kweli kwa Mbunge huyo baada ya jana Jumamosi ya Machi 21, kupokelewa rasmi na chama hicho na kukabidhiwa kadi yake yenye namba 007194.
Zitto akionyesha kadi yake kwa wanachama wa ACT.(P.T)
Hii inafuatia siku moja baada ya Zitto kutangaza kuachia ubunge na kuandika barua rasmi ambapo sasa amekuwa mwanachama wa ACT-Tanzania na kuahidi kuendeleza mapambano ndani ya chama hicho.
Kadi ya Zitto Kabwe yenye namba 007194.
Hata hivyo, kwa mujibu wa viongozi waandamizi wa ACT-Tanzania wamedokeza kuwa, Zitto ataongea na vyombo vya habari leo Jumapili ya Machi 22.
Zitto Kabwe akivalishwa skafu ya ACT mara baada ya kupokea rasmi kadi ya chama hicho jana.
ACT-Tanzania: kirefu chake ni : Chama cha Alliance for Change and Transparence (ACT-Tanzania). Makao makuu ya chama hicho yapo Kijitonyama Jijini Dar es Salaam, Tanzania.
CREDIT: Modewji Blog
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company