Mchambuzi Mkuu wa Mifumo ya Komputa wa Tume ya Taifa ya kudhibiti Ukimwi (DCC), January Ntisi akizindua kitabu cha ripoti ya Bodi ya Kupambana na Dawa za Kulevya ya Umoja wa Mataifa, kwenye hafla ya uzinduzi uliofanyika Machi 4, MAELEZO, jijini Dar es salaam. Kushoto ni Afisa Mipango wa Umoja wa Mataifa, Immaculata Malyamkono-Nyoni na katikati ni Makamu Mwenyekiti wa Mtandao wa Kupambana na Watumiaji wa Madawa ya Kulevya,Very Kunambi. (Picha na Andrew Chale).
Afisa habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Stella Vuzo akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na uzinduzi wa ripoti ya Kupambana na dawa za kulevya ya Umoja wa Mataifa. Kulia ni mgeni rasmi Mchambuzi Mkuu wa Mifumo ya Kompyuta wa Tume ya Taifa ya kudhibiti Ukimwi (DCC), January Ntisi na kushoto ni Afisa Habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Usia Nkhoma Ledama.
Uongozi wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataaifa (UNIC) umezindua ripoti ya Kupambana na dawa za kulevyaa ya Umoja wa Mataaifa, Uzinduzi uliofanywa Machi 4, Jijini Dar es Salaam.
Wakizungumza mbele ya wandishi wa habari kwa upande wake, Afisa Habari wa Kituo Cha Habari wa Umoja wa Mataifa (UNIC), Stella Vuzo alibainisha ripoti hiyo imeweza kuchambua mambo mbalimbali dhidi ya dawa za kulevya na mikakati iliyofikiwa.
Ambapo alisema kuwa miongoni mwa mambo yaliyomo kwenye ripoti hiyo ni pamoja na kupungua kwa wimbi la kuingia kwa dawa za kulevyaa nchini hasa kupitia njia za bahari ya Hindi huku mji wa Mexico wa America, ukipunguza kwa asilimia kubwa matumizi ya dawa za kulevya.
Vuzo alibainisha kuwa, pia mikakati iliyofikiwa ambayo pia imo kwenye ripoti hiyo ni pamoja na mfumo wa kuwasaidia watumiaji wa dawa za kulevya wanaoacha kwa kuwapatia dawa maalum za kupunguza taratibu matumizi hayo.
'Mipango ya kuwapatia wale wanaocha dawa maalum za kusaidia utumiaji wa madawa na pia dhidi ya kupambana na dawa maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi wa watumiaji" alisema Vuzo. Aidha, alibainisha kuwa, Afrika Kusini katika bara la Afrika ndio inayoongoza kwa kuwa na njia nyingi za usafirishaji wa dawa za kulevya aina ya Cocaine na Heroine .
Mchambuzi Mkuu wa Mifumo ya Kompyuta wa Tume ya Taifa ya kudhibiti Ukimwi (DCC), January Ntisi akionyesha ripoti hiyo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani).
Kwa upande wake Mchambuzi Mkuu wa Mifumo ya Kompyuta wa Tume ya kudhibiti Ukimwi DCC, January Ntisi ,amesema wanashirikiana katika kupambana na dawa za kulevya na umoja huo kwani Tanzania ni miongoni nchi ambazo pia zinakabiriwa na tatizo hilo.
Alisema mwaka jana walikamata dawa tani 2.3 ambazo zingeingia nchini kungekuwa na kundi kubwa ambao wanatumia dawa hizo.
Kwa upande wake, Immaculate Nyoni ambaye ni Project officer UNODC alibainisha juhudi mbalimbali zinafanywa katika kukabiliana na wimbi la dawa za kulevya duniani kote ambapo kwa sasa angalau matumizi hayo yakiendelea kupungua.
Mchambuzi Mkuu wa Mifumo ya Kompyuta wa Tume ya Taifa ya kudhibiti Ukimwi (DCC), January Ntisi akifafanua jambo na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi huo.
Baadhi ya waandishi wa habari na wadau wa kupambana utumiaji wa Madawa ya Kulevya waliohudhuria uzinduzi huo.
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago