KWA UFUPI
Wakizungumza kwa nyakati tofauti siku moja baada ya mwanasiasa huyo kufukuzwa, baadhi ya wanasiasa walisema kuwa CCM imefanya kosa kwa kutompa nafasi ya kujitetea juu ya tuhuma zilizokuwa zinamkabiliMkurugenzi wa Uenezi na Mawasiliano ya Umma wa CUF, Salim Bimani alisema kitendo cha CCM kumfukuza Moyo kinaonyesha jinsi kilivyopoteza mwelekeo kwa kukosa viongozi bora. Alieleza kushangazwa kwake na hatua hiyo ya kumfukuza Moyo licha ya mchango wake mkubwa katika harakati za ukombozi wa Zanzibar.
Bimani alisema kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kila Mtanzania ana haki ya kutoa maoni yake na hatua ya kumfukuza kutokana na kutofautiana kimtazamo kuhusu mfumo wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, haikuwa mwafaka katika misingi ya utawala bora.
Moyo ajibu
Akizungumzia kutimuliwa kwake, Moyo alisema ataendelea kutetea mfumo wa Muungano wa Serikali tatu hadi Zanzibar itakapofanikiwa kupata mamlaka kamili ya kujitawala na kujiamulia mambo yake kama ilivyokuwa kabla ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964 licha ya kufukuzwa CCM juzi.
Mkurugenzi wa Uenezi na Mawasiliano ya Umma wa CUF, Salim Bimani alisema kitendo cha CCM kumfukuza Moyo kinaonyesha jinsi kilivyopoteza mwelekeo kwa kukosa viongozi bora. Alieleza kushangazwa kwake na hatua hiyo ya kumfukuza Moyo licha ya mchango wake mkubwa katika harakati za ukombozi wa Zanzibar.