Wadau wa mapambano ya kudhibiti vifo vya mama na mtoto chini ya umri wa miaka mitano mkoani manyara wametoa mapendekezo ya kudhibiti vifo hivyo kwa kuitaka serikali kuongeza bajeti kwa mwaka ujao wa fedha ili kutoa nafasi kwa vituo 140 vya afya ya msingi ambavyo havitoi huduma yeyote ya dharura ya uzazi kamilifu,huku pia wakiwataka madiwani kuisaidia serikali kuwahamasisha wanaume kuokoa vifo hivyo kuhudhuria kliniki mara kwa mara na wake zao.
Mapendekezo hayo wameyatoa baada ya kusikia hali tete inaoukabili mkoa wa Manyara unaoonekana kuwekwa kwenye alama nyekundu iliyo hatarishi kwenye mazingira ya vifo hivyo hapa nchini,hasa pale ilipobainika kuwa hata huduma jumuishi kwenye mazingira ya vijijini hazina tija sambamba na kiwango cha watoto wanaozaliwa na akinamama wenye VVU na kupata dawa za (ARV'S) za kufubaza VVU hazifiki hata asilimia 23 ya huduma na hatari kwa vifo hivyo.
Nayee mganga mkuu mkoani manyara Dr. Ali Bin Uledi katika taarifa yake kwa wadau hao amekiri kuwepo kwa vifo 665 vya watoto chini ya umri wa miaka mitano hadi kufikia mwaka 2014 vinavyochangiwa na uhaba wa huduma ya uzazi wa mpango,watendaji kukosa weledi,na hakuna hospitali hata moja yenye utaratibu wa kutoa dawa zenye kukomaza mapafu ya mtoto mtarajiwa kwa mama aliyepatwa uchungu wa kujifungua.
Hata hivyo mkuu wa mkoa wa manyara Dr.Joel Nkaya Bendera maarufu kama"KOCHA"aliyeonekana kushtushwa na changamoto ya vifo hivyo huku mkoa wake ukiwa kwenye kiashiria cha alama nyekundu amesema ingawa sababu kubwa inayochangia ni kutowajibika kwa watendaji,lakini ni lazima sasa kuwepo kwa jitihada za kupunguza vifo vya mama kutoka vifo 34 na vile vya watoto kwa kila mmoja akiwajibika,kabla ya kugawa azimio la uwajibikaji na mkakati. (KILONGE)
#USOPEN_VIGOGO CHALI
-
SIKU Safi kwa Muaustralia Nick Kyrgios baada ya ushindi dhidi Johnson na
kutinga raundi ya Pili.
- Rafael Nadal akimchapa Millman Seti Tatu zote mfululi...
5 years ago