Mkuu wa Wialaya ya Kinondoni Mh Paul Makonda akikagua Mazingira ya Soko la Mahakama ya Ndizi lililopo Mabibo akiwa ameambatana na Viongozi wa wafanyabiashara wa soko hilo alipofika kusikiliza kilio chao. Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ametembelea Soko hilo baada ya viongozi wa soko hilo kufikisha kilio chao cha muda mrefu kwake.
Mkuu wa Wialaya ya Kinondoni Mh Paul Makonda Akipatiwa Maelezo zaidi kuhusu eneo la Soko hilo kutoka kwa Mwenyekiti wa Soko Hilo Ndugu Idd Pazi kwa niaba ya Wafanyabiahara wa Soko Hilo.
Mkuu wa Wialaya ya Kinondoni Mh Paul Makonda Akizungumza na wafanyabiashara wa soko la Ndizi lililopo Mabibo, akiwaambia amepokea kwa mikono miwili kilio chao na kwamba atalifanyaia kazi kwa haraka kwa kushirikiana na ngazi mbalimbali za maamuzi na mapema atawajibu.Mkuu wa Wilaya huyo amesema ni ngumu sana kwake kutoa ahadi ambayo itakuwa ngumu kutekelezeka kwa kuwa eneo hilo ni Mali ya Kiwanda cha Urafiki na kiwanda kimebinafsishwa hivyo ni ngumu kuahidi kama watalipata eneo hilo kwa ajili ya Soko Bila kujua Mipango ya Kiwanda kuhusu eneo hilo.
Baadhi ya Wafanyabiashara wa Soko hilo wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Wialaya ya Kinondoni Mh Paul Makonda Wakati ikajibu baadhi ya Kero za wafanyabiashara hao.
Mkuu wa Wialaya ya Kinondoni Mh Paul Makonda Akipokea Baadhi ya Zawadi alizopewa na wafanyabiashara wa Soko la Mahakama ya Ndizi la Mabibo.
Wafanyabiashara hao kilio chao kikubwa kwa Mkuu wa wilaya hawajui hatma ya biashara yao Sokoni hapo kwa kuwa eneo wanalofanyia biashara sio rasmi kwajili ya soko bali ni Mali ya Kiwanda cha Urafiki.Wafanyabiashara haowamesema Kutokana na kutokutambulika kwa eneo hilo kama eneo la soko kunawanyima fursa mbalimbali ikiwemo Mikopo. Wafanyabiashara ambao wapo takribani 1,000 walisema wako hapo kwa muda mrefu lakini hawajui hatma ya maisha yao, na kwamba miundombinu ya Soko haifai kabisa.
Mh Paul Makonda alitumia mkutano huo na Wafanyabiashara kuwaeleza mipango na mikakati yake iliyokwisha kuanza na ambayo ataianzaisha hivi karibuni kwa ajili ya Kutatua kero zinazowakabili wakazi wa wilaya ya Kinondoni. Akieleza Zaidi Mh Makonda amesema kwenye ofisi yake kila siku ya Jumanne ni siku ya Kumwona Mkuu wa Wilaya kwa hiyo ametoa rai wa wakazi wote wa kinondoni wenye matatizo Mbalimbali Kufika ofisini kwake kila Jumanne kumwona. Pia kwa wale wakazi wa Kinondoni wenye migogoro ya Ardhi kufika ofisini kwake kila siku ya Ijumaa kwa ajili ya kutatua kero za wana- Kinondoni
#USOPEN_VIGOGO CHALI
-
SIKU Safi kwa Muaustralia Nick Kyrgios baada ya ushindi dhidi Johnson na
kutinga raundi ya Pili.
- Rafael Nadal akimchapa Millman Seti Tatu zote mfululi...
5 years ago