Mali: Abdelkrim al-Targui auawa

Wanajeshi wa Ufaransa wa kikosi cha Barkhane katikati mwa mji wa Gao.
RFI/David Baché
Na RFI
Taarifa ya RFI. Mwanajihadi Abdelkrim al-Targui ameuawa katika shambulio la wanajeshi wa Ufaransa lililoendesha kaskazini mashariki mwa Mali. Abdelkrim al-Targui amekua akihusishwa katika visa mbambali vya utekaji nyara kwa raia wa Ufaransa nchini Mali.
  Abdelkrim al-Targui alikiri kwa niaba ya kundi lake kuwateka nyara na kuwaua maripota wa RFI Ghislaine Dupont na Claude Verlon,Novemba 2 mwaka 2013.

Opereshini hiyo iliendeshwa Jumatatu jioni wiki hii na vikosi maalumu vya Ufaransa kaskazini mwa Mali. Katika tangazo lililotolewa Jumatano wiki hii, wizara ya ulinzi ya Ufaransa imebaini kwamba wanajihadi wanne wameuwawa, ikiwa ni pamoja na Abdelkrim al-Targui na Ibrahim Ag Inawalen, ambao walikua viongozi muhimu wa kundi la Ansar Dine na Al Qaeda

Abdelkrim al-Targui, ambaye jina lake halisi ni Hamada Ag Hama, alikuwa mmoja wa waliokua wakilengwa na mashambulizi ya jeshi la Ufaransa tangu kuanzishwa kwa operesheni ya kijeshi iitwayo Serval mwezi Juni mwaka 2013. Abdelkrim al-Targui alikuwa kiongozi wa moja ya makundi manne ya Aqmi, kama alivyokuwa pia Abu Zeid.

Hamada Ag Hama na watu wa kundi lake la Al-Ansar walikua wakijihusisha na visa vya utekaji nyara kwa raia wa Ufaransa katika eneo hilo la kaskazini mashariki mwa Mali.

Raia wa Ufaransa walitekwa nyara na kuuawa katika ukanda huo ni pamoja na Michel Germaneau, aliyetekwa nyara mwaka 2010 kaskazini mwa Niger, na baadaye aliuawa na mtu anayeshukiwa kuwa Targui. Serge Lazarevic na Philippe Verdon, ambao walitekwa nyara katika kijiji cha Hombori mwaka 2010. Utekaji nyara ambao ulidaiwa kutekelezwa na kundi la Abdelkrim al-Targui.

Novemba 2 mwaka 2013, mwaandishi wa habari Ghislaine Dupont na fundi mitambo Claude Verlon, walitekwa nyara nyara katika mji wa Kidal na kuuawa dakika thelathini baadaye kwenye umbali wa kilomita 12 na mji huo. Siku nne baadaye, kundi la Abdelkrim al-Targui lilikiri kuhusiika na mauaji hayo.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company