''MAPINDUZI BURUNDI''

Mnamo 13 mwezi May jenerali mmoja wa jeshi alitangaza katika redio ya taifa kwamba rais wa Burundi amepinduliwa na kwamba serikali ya mpito itabuniwa.Lakini msemaji wa rais alikana habari hizo akidai kuwa kulikuwa na usaidizi mdogo katika jeshi kwa mapinduzi kutendeka.Rais Nkurunziza alidaiwa kurudi nchini Burundi kutoka Tanzania ,lakini imethibitishwa kuwa leo, alishindwa kufanya hivyo na kwamba yungali nchini Tanzania.
21.15pm:-Nkurunziza hayuko Tanzania,Je Yuko wapi?
Rais Nkurunziza

Msemaji wa rais Nkurunziza Willy Nyamitwe amezungumza na mwandishi wetu na kuthibitisha kuwa Nkurunziza aliondoka nchini Tanzania siku ya jumatano lakini hawezi kubaini iwapo yuko nchini Burundi au la.Amesema kuwa kutokana na maswala ya usalama hawezi kutaja mahala alipo lakini yu buheri wa afya.


20.25pm-Jenerali Godefroid NiyombareJenerali Godefroid

Jenerali aliyetangaza mapinduzi .





20.28pm-Wanajeshi watiifu wa NkurunzizaMji wa Bujumbura

Wanajeshi walio watiifu kwa rais Pierre Nkurunziza wametangaza kudhibiti maeneo muhimu ya mji mkuu wa Bujumbura siku moja baada ya jaribio la mapinduzi.Kulikuwa na mapigano makali mjini Bujumbura,hususan katika kituo cha habari cha kitaifa,lakini makabiliano hayo yameisha huku wanajeshi watano wakidaiwa kuuawa.
18.05pm-Wanajeshi watiifuWanajeshi watiifu wapiga doria Bujumbura

Makundi hasimu ya jeshi la Burundi yamekuwa yakipambana kukidhibiti chombo cha kitaifa cha habari RTBN ambacho kilizimwa kwa mda .Duru zimearifu kuwa kituo hicho cha habari kiko chini ya udhibiti wa vikosi vinavyomtii rais Pierre Nkurunziza.

17.53pm-Viongozi wajadili BurundiBaraza la usalama la umoja wa Afrika laijadili Burundi kwa sasa

Baraza la usalama la umoja wa Afrika limetuma ujumbe katika mtandao wake wa Twitter likisema kuwa wanachama wa baraza hilo kwa sasa wanaijadili.

17.00pm-Wanajeshi wapiga doriaMaafisa wa polisi wapiga doria Burundi

Maafisa wa polisi waliojihami katika mji mkuu wa Burundi,Bujumbura wanaonekana wakilinda vizuizi vya barabarani leo

16.50pm-Mkutano kuhusu Burundi waendelea.Mkutano wa baraza la usalama la Umoja wa Afrika

Baraza la usalama la umoja wa Afrika kwa sasa linaijadili Burundi.

tweets: "Chini ya Uongozi wa balozi Amina Diallo wa Niger,ni mkutano wa 507.Baraza hilo linaangazia hali ilivyo Burundi

16.10pm-RNTB yarudisha matangazoKituo cha redio

Kituo cha redio cha Burundi RNTB kimerudi hewani,chini ya wanajeshi walio watiifu kwa rais Pierre Nkurunziza kulingana na duru kutoka kwa wanajeshi.Tumethibitisha kuwa kimeanza kurusha tena matangazo.

15.50pm-Nkurunziza asema yuko tayari kusameheRis wa Burundi Pierre Nkurunziza

Shirika la habari la Reuters limenukuu baadhi ya mahojiano yaliofanywa na rais Nkurunziza na kituo cha habari cha RTNB mapema leo.

''Ninalishtumu kundi lililopanga mapinduzi'',alinukuliwa akisema.

''Nwashkuru wanajeshi wanaorudisha hali ya kawaida na namsamehe mwanajeshi yoyote ambaye yuko tayari kusalimu amri''.

Lakini baada ya mahojiano hayo kulikuwa na vita karibu na kituo hicho cha habari ambacho kwa sasa kimezimwa.

15.47pm-Ramani ya BurundiRamani ya Burundi

Ramani ya taifa la Burundi.
15.45pm-Mji wa BujumburaBurundi

Mji wa Burundi Bujumbura ulivyo kwa sasa

15.30pm-Vyombo vya habari vyazimwaKItuo cha habari cha Isanganiro

Kituo cha habari cha Burundi Isanganiro kimesema kuwa kimefungwa na vituo vyengine vya kibinafsi .Kituo hicho ni miongoni mwa vile vilivyotangaza mapinduzi siku ya jumatano.

15.17pm-Kituo cha habariAskari Burundi

Kituo cha habari cha Redio ya RTNB kimezimwa kufuatia mapigano makali karibu na afisi zake mjini Bujumbura.

15.01pm:Rais wa Burundi AhojiwaWanajeshi nchini Burundi wakipiga doria

Kituo cha habari cha Burundi RTBN kimemhoji rais Pierre Nkurunziza kwa simu mwendo wa saa sita.Vita vimezuka karibu na afisi za kituo hicho cha habari.Jenerali anayeunga mkono jaribio hilo la mapinduzi amekiambia chombo cha habari cha AFP kwamba vitengo vinavyopigana kumpindua vimepata agizo la kukiteka kituo hicho habari cha RTNB kwa kuwa wana uwezo.

14.30pm:Makundi ya vijana waliojihamiVijana Burundi

Kuna madai kwamba kundi la vijana linalunga mkono serikali limeshambulia kituo kimoja cha habari cha kibinafsi mjini Bujumbura.KUndi hilo linalojulikana kama Imbonerakure,baadhi ya watu wanaamini kwamba vijana hao wanatumiwa kama wapiganaji na kwamba huenda wamepewa silaha ili kuwatishia raia kabla ya uchaguzi.

13.45pm-Hali ni tete BurundiWanajeshi wa BUrundi

Hali bado ni tete nchini Burundi siku moja tu baada ya jenerali mmoja wa jeshi kujaribu kutekeleza mapinduzi .Barabara nyingi zimeendelea kuwa bila watu kwa kipindi kirefu cha alfajiri huku wengi wakisalia ndani ya majumba yao wakihofia usalama kulingana na mwanahabari wetu Ruth Nesoba.

13:30pm-UkabilaKiongozi wa jeshi aliyetangaza mapinduzi

Tofauti zilizopo katika jeshi la Burundi kufuatia jaribio la mapinduzi hazionekani kuwa katika misingi ya kikabila ,mkuu wa majeshi ambaye ni mtiifu kwa rais Nkurunziza pamoja na jenerali wa majeshi aliyetangaza mapinduzi hayo ni wa kabila la Hutu.Makundi hayo yanaonekana kugawanyika kati ya wale wanaoamini rais Nkurunziza alikiuka makubaliano ya amani yaliomaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa kutaka kuongoza kwa muhula wa tatu na wale wanaosalia kuwa watiifu kwake

12:05pm-Wanajeshi watiifuMj wa Burundi Bujumbura

Afisa mmoja wa kijeshi ameiambia BBC Afrique kwamba wanajeshi watiifu nchini Burundi wanadhibiti mji wa Bujumbura ,uwanja wa ndege,makao ya rais pamoja na vituo vya redio na runinga.

12:00pm-Milio ya RisasiWanajeshi wa Burundi

Makundi hasimu ya askari yanakabiliana katikati mwa mji mkuu wa Burundi- Bunjumbura, mahala ambapo tangazo lilitolewa jana Jumatano kuwa Rais Pierre Nkurunziza, amepinduliwa.

Makabiliano ya risasi yanaendelea kwa sasa, huku milipuko kadhaa ikisikika.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company