John Kerry akisikiliza kwa makini masuala yaliyokuwa yanazungumzzwa
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani John Kerry,amesema kwamba amekuwa na mazungumzo ya kirafiki kuhusiana na mzozo wa Ukraine pamoja na mambo mengine na mwenyeji wake rais wa Urusi , Vladimir Putin, katika ghuba ya bahari ya shamu pwani ya Sochi.
Lakini pia Kerry alikutana na waziri wa masuala ya mambo ya kigeni wa Urusi, Sergei Lavrov, katika ziara yake ya kwanza tangu mgogoro wa Ukraine ulipoanza mwaka wa jana.
Kerry pia hakusita kuzungumzia masuala ya ziada ambayo yalijiri katika mazungumzo yao kwamba ni juu ya yanaoendelea baina ya Iran na Syria. Amesema kwamba ni muhimu kuzingatia makubaliano waliyofikia baina ya Marekani na Urusi wakati wakiangazia masuala mengine yanayo ikabili dunia.
Mapema kabla ya kuanza mazungumzo hayo, waziri huyo ma mambo ya nchi za nje wa Marekani, alipata fursa ya kuweka shada la maua katika makaburi ya askari waliopigana vita vikuu vya pili vya dunia mjini Sochi. Uhusiano baina ya Urusi na Marekani umeshuka kwa kasi baada ya Urusi kujihusisha harakati za krimea na kuwaunga mkono wapiganaji wa waasi walioko upande wa Mashariki mwa Ukraine.
#USOPEN_VIGOGO CHALI
-
SIKU Safi kwa Muaustralia Nick Kyrgios baada ya ushindi dhidi Johnson na
kutinga raundi ya Pili.
- Rafael Nadal akimchapa Millman Seti Tatu zote mfululi...
5 years ago