Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimkabidhi pikipiki Mratibu wa Elimu wa Kata ya Ibiwhwa wilayani Bahi, Jacob Mwakalambo ikiwa ni chombo cha kumwezesha kutekeleza majukumu yake katika maadhimisho ya wiki ya elimu wenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma Mei 15, 2015. Kulia ni Naibu waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Kassim Majaliwa.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na mzee wa Kihadzabe, Mandona katika maonyesho ya wiki ya Elimu kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma Mei 11, 1015. Kulia ni Bibi Agnes Israel. (kilonge)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipata maelezo kuhusu shughuli mbalimbali za British Council wakati alipotembelea banda la Taasisi hiyo kwenye maonyesho ya Elimu aliyoyafungua kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma Mei 11, 2015.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizazama madawati ya gharama nafuu wakati alipotembelea Edosama Hardware watengenezaji wa madawati ya gharama nafuu baada ya kufungua wiki ya elimu kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma Mei 11, 2015. Kuliani Oscar Kaduma na wapili kulia ni Edward Maduhu wote wakiwa ni watendaji wa kampuni hiyo. Kushoto ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, KassimMajaliwa.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimsikiza mtoto wa kabila la Wahadzabe,, Kone Paschal wa darasa la kwanza katika shule ya msingi ya bweni ya Mngulu mkoani Singida katika maonyesho ya wiki ya Elimu kwenye uwanja wa Jamhuri Dodoma Mei 11, 2015/(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).