RAIS WA MSUMBIJI FELIPE JACINTO NYUSI ALIHUTUBIA BUNGE DODOMA

Rais Wa Msumbiji Felipe Jacinto Nyusi akilihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo mjini Dodoma huku Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Spika wa Bunge hilo Mh.Anna Makinda wakisikiliza.



Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Rais wa Msumbiji Felipe Jacinto Nyusi,Waziri Mkuu Mizengo Pinda,Spika wa Bunge la Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania na viongozi waandamizi katika serikali ya Msumbiji wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya Rais wa Msumbiji kulihutubia Bunge lao mjini Dodoma.



Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikweteakimtambulisha katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwa Rais wa Msumbiji Felipe Jacinto Nyusi wakati Rais huyo wa Msumbiji alipowasili katika makao makuu ya CCM m.Jakayajini Dodoma na kuzungumza na viongozi waandamizi .Kushoto ni Naibu katibu Mkuu wa CCM Bwana Mwigulu Nchemba.



Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania Mh.Anna Makinda akimkaribisha Rais wa Msumbiji Felipe Jacinto Nyusi katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma ambapo Rais huyo alilihutubia Bunge hilo.



Rais Wa Msumbiji Felipe Jacinto Nyusi akipokea heshima muda mfupi baada ya kuwasili katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma akisindikizwa na mwenyeji wake Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete.



Rais wa Msumbiji Felipe Jacinto Nyusi akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo huku Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Spika Mhe.Anna Makinda wakishuhudia. (Picha na Freddy Maro)
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company