Uchaguzi Uingereza: Chama cha Conservative chaongoza

Maafisa wa uchaguzi wakibeba masanduku ya kura katika kituo cha kuhesabu kura katika mji wa Doncaster, Mei 7 mwaka 2015.
REUTERS/Darren Staples
Na RFI

Nchini Uingereza, vituo vya kuoigia kura vimefungwa rasmi saa tano usiku wa kiuamkia leo Ijumaa saa za Afrika ya Kati. Kulingana na matokeo ya mwanzo ya uchaguzi, chama cha Conservative kinaongoza katika uchaguzi huo mkuu, bila hata hivyo kupata uingi wa viti katika baraza mbili za Bunge na Seneti.
     Kulingana na makadirio hayo yaliyotangazwa na televisheni za Uingereza, chama cha Conservative cha waziri mkuu anayemaliza muda wake, David Cameron, kwa wakati huu kinaongoza kwa uchaguzi huo. Chama hicho kwa sasa hakitosubiri uingi wa viti 326 katika Baraza la Bunge. Uchunguzi uliyoendeshwa katika vituo 140 kupitia wapiga kura 20,000 unaonyesha kuwa chama cha Conservative hakitakua na wabunge wengi.

Chama cha Conservative kinasadikiwa kuwa huenda kikapata viti 316, ikilinganishwa na miaka mitano iliyopita. Chama cha Labour cha Ed Miliband huenda kikapata viti 239, ikimaanisha kuwa kimepungukiwa na viti 19 ikilinganishwa na uchaguzi mkuu uliyopita. Chama cha Nick Clegg kinasadikiwa kupata viti 10 pekee, huku chama cha SNP kikisadikiwa kupata viti 58 kwa jumla ya viti 59 katika jimbo la Scotland. Chama cha SNP huenda kikapata uingi wa viti katika jimbo hilo la Scotland. Chama cha Kijani pamoja na chama cha Ukip vinasadikiwa kupata viti 2 kwa kila chama.

" Kama kweli uchunguzi huu ni sahihi, ina maana kwamba chama cha Conservative kimeibuka mshindi katika uchaguzi, huku chama cha Labour kikipoteza. Hatujaona serikali inayemaliza muda wake ikipata uingi wa viti kwa njia hii tangu mwaka 1983 ", amekaribisha Michael Gove, msemaji wa chama cha Conservative.

" Hii itakuwa kura isiyokuwa ya kawaida ya imani kwa David Cameron na kwa ujumbe wetu, ambao ni kama watu wanataka kupata ahueni katika sekta ya Uchumi, ni lazima wahakikishe kwamba David Cameron anapaswa kuendelea kushikilia wadhifa wake wa Waziri mkuu ", ameendelea kusema Maichael Gove.

Upande wa Kazi wa chama cha Labour wanabaini kwamba uchunguzi huo unatia wasiwasi na unatoa viti vichache kwa chama cha Labour ikilinganishwa na mwaka 2010.

" Kama kweli makadirio hayo ni ya kweli, ina maana kwamba chama cha Conservative kimepoteza uingi wa viti unaokipelekea kuunda muungano. Swali ni (...) kama Chama cha Conservative kinaweza kuunda idadi kubwa ya wabunge katika Bunge jipya", ameuliza Harriet Harman, Naibu Mwenyekiti wa chama cha Labour.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company