Bw. Salum anayesakwa na polisi kwa tuhuma za kumbaka na kumpachika mimba binti yake wa kambo.
Waandishi wetu
MUNGU wangu! Mwanaume mmoja mkazi wa Mwenge jijini Dar es Salaam aliyefahamika kwa jina moja la Salum, anasakwa na polisi kwa tuhuma za kumbaka na kumpa ujauzito bintiye wa kambo (jina limehifadhiwa).
Binti anayedaiwa kubakwa na kusababishiwa ujauzito na baba huyo.
Chanzo cha kuaminika kililiambia gazeti hili kuwa mwanaume huyo alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanaye kwa muda mrefu, lakini iligundulika hivi karibuni baada ya wawili hao kufanya jaribio la kutoa mimba hiyo ili msichana huyo aendelee na masomo katika shule moja ya sekondari iliyopo mkoani Iringa.
Mama wa binti huyo, Prisca Steven. (Dk)
Mama wa binti huyo, Prisca Steven (32) alikiri kutokea kwa tukio hilo na kusema licha ya kupata aibu kubwa, lakini pia mwanaume huyo ameharibu maisha ya mtoto wake kwa kumkatisha masomo. Alisema kwa sasa mumewe huyo amekimbia nyumbani na amekuwa akimtumia sms za vitisho au kuomba afute kesi hiyo ili kuepuka kifungo cha miaka 30 jela endapo atakutwa na hatia.
Mama na Baba wakiwa katika picha ya pamoja.
Kwa upande wake, mwanaume huyo alipoulizwa kwa njia ya simu, alikana kuhusika na tukio hilo akisema hausiki na kwamba hajakimbia nyumbani kwake isipokuwa alipata safari ya kikazi huko Zanzibar. Jalada la shauri hilo limefunguliwa katika Kituo cha Polisi Kijitonyama ‘Mabatini’ kwa nambari KJN/RB/6485/15 KUBAKA
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago