Kumekuwa na taarifa za kuweko watu wanaotaka kushambulia Burundi hali iliyozidisha kasi ya watu wanaotoroka nchi.
kulia- Ris wa Burundi Piere Nkurunzinza
Chama tawala nchini Burundi kinaomba uchuguzi ufanyika juu ya taarifa za kuwepo mafunzo ya kijeshi kwa wakimbizi wa Burundi waliokimbilia katika nchi jirani za Rwanda Tanzania na Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo kwa nia ya kuivamia Burundi na kuvuruga uchaguzi mkuu nchini humo.
Kumekuwa na taarifa za kuweko watu wanaotaka kushambulia Burundi hali iliyozidisha kasi ya watu wanaotoroka nchi.
Hayo yalikuwa katika tangazo lenye ukurasa 9 lililotolewa Alhamisi usiku na chama hicho.
Tangazo hilo lina lengo la kuelezea msimamo wa chama hicho kuhusu maamuzi ya mkutano wa umoja wa afrika uliofanyika jijini Johanesbourg nchini Afrika ya kusini.
Miomgoni mwa maamuzi ya mkutano huo ni kuwata wadau wa uchaguzi wa Burundi warejee kwenye meza ya mazungumzo.Umoja wa afrika ulieleza kuwa utawatuma watalaam wa kijeshi ambao watajihusisha na kuwapokonya silaha watu wanazozimiliki kinyume cha sheria na kuomba mazungumzo kwa ajili ya kumaliza mgogoro huu wa kisiasa yaanze upya.
Wakati huo huo, Mwanasheria aliyeteuliwa kuziba nafasi ya kurejelea mjumbe wa korti ya katiba aliyetoroka nchi baada ya kukataa kuidhinisha rais wa Burundi kuwa ana haki ya kugombea muhula wa tatu amekula kiapo hii leo mbele ya rais wa Burundi Pierre Nkurunziza. Bwana Benoit SIMBARAKIYE pamoja na mjumbe mwingine wa korti hiyo wameahidi kufanya kazi bila kuegamia upande wowote na kuheshimu makubaliano ya umoja wa warundi.
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago