Burundi: mvutano wa kisiasa na vurugu mpya zaibuka Bujumbura

Askari polisi apiga doria katika mitaa ya Bujumbura, mji mkuu wa Burundi, mwishoni mwa mwezi Julai.
REUTERS/Mike Hutchings
Na RFI

Hali ya wasiwasi imeendelea kutanda nchini Burundi hususan katika mji mkuu wa Bujumbura. Alhamisi wiki hii, watu wanne waliuawa katika wilaya mbili ambazo ni kitovu cha maandamano ikiwa ni pamoja na Cibitoke pamoja na Buterere, jijini Bujumbura.

Mashambulizi ya hivi karibuni dhidi ya watu walio kwenye mstari wa mbele yameendelea kutia hofu kwa kutokea mashambulizi zaidi na ulipizaji kisase. Hali ya wasiwasi imenea katika nyanja zote, mitaani kama katika mzunguko mzima wa kisiasa nchini humo.

Jumatano usiku wiki hii, wakimbizi wawili kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo waliuawa kwa kupigwa " risasi " wilayani Cibitoke. wakaazi wa wilaya hiyo wamesema kuwa raia hao " walilazwa chini na polisi, na kisha kuwafyatulia risasi nyingi ".

Baadhi ya mashahidi wanahisi kwamba wakimbizi hao kutoka Congo huenda waliuawa kutokana na kushiriki kwao katika maandamano yaliofanyika miezi miwili iliopita mjini Bujumbura. " Huo ni uzushi ", amesema afisa mmoja wa polisi, huku akibaini kwamba "Katika eneo hilo, ni siku nne mfululizo kila jioni askari polisi wamekua wakilengwa na mashambulizi ya risasi au gruneti, hata Jumatano jiuoni wiki hii, kuna askari polisi aliyejeruhiwa", ameongeza afisa huyo wa polisi.

Alhamisi asubuhi, Agosti 6, wapita njia waligundua miili mingine miwili wilayani Buterere, sehemu nyingine ya ya waandamanaji. Watu wawili walipatikana wameuawa mikono yao ikifungwa kamba, mmoja alikuwa na mfuko kichwani.

" Hakuna aliye weza kuwatambua. Watu hao waliuawa mahali pengine na kuletwa kutupwa hapo ili kuwatia uoga wakaazi wa wilaya ya Buterere", mmoja wa mashahidi amesema.

" Kwa sasa sitoki nje ya nyumba yangu ", amesema mwanasiasa mmoja kutoka chama cha upinza. " Tangu tuhudhuriye mkutano wa Addis Ababa, majina yetu yamewekwa kwenye orodha ya watu wanaotafutwa ili waeweze kuuawa ", akimaanisha mkutano wa Addis Ababa uliokua nalengo la kuunda taasisi za uongozi sambamba na serikali ya Burundi zitakazo wajumuisha wapinzani kutoka ndani na nje ya nchi ya Burundi.

Mpinzani mwingine, Jean Minani alishangaa kuwapoteza walinzi wake. " Jean Minani ni spika wa zamani wa Bunge, na anahaki ya kupata walinzi ", amesema mshirika wake wa karibu.

Naibu msemaji wa polisi wakati huo huo ametangaza kwenye redio ya taifa kwamba viongozi watano wa serikali tano wameshauawa tangu Jumamosi. " Wamejaribu kutuangamiza moja kwa moja ", amesema afisa mmoja wa serikali ya Burundi, akinyooshea kidolea cha lawama upinzani.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company