JKT yajidhatiti kutoa elimu ya ujasiriamali kwa vijana

Jeshi la kujenga taifa JKT limesema limejizatiti kutoa elimu ya ujasiriamali, uzalendo na elimu ya kujitegemea kwa vijana wanaojiunga na jeshi hilo kwa kujitolea
Mkuu wa Mafunzo na Utawala wa Jeshi la kujengaTaifa (JKT) Brigedia Jenerali Jacob Kingu akiongea na waandishi wa habari

Jeshi la kujenga taifa JKT limesema limejizatiti kutoa elimu ya ujasiriamali, uzalendo na elimu ya kujitegemea kwa vijana wanaojiunga na jeshi hilo kwa kujitolea na kwa mujibu wa sheria ili kuhakikisha wanapohitimu na wanakuwa na ujuzi wa kuwawezesha kujiajiri na kujitegemea wenyewe.

Hayo yamesemwa mkoani PWANI na mkuu wa utawala na mafunzo wa jeshi la kujenga taifa Brigedia Jenerali JACOB KINGU wakati zaiara ya siku moja ya waandishi wa habari waliotembelea kikosi namba 832 KJ RUVU JKT kujifunza kazi mbalimbali zinazofanywa na jeshi hilo.

Amesema kuhakikisha kuwa dhamira ya kurejesha jeshi hilo kwa vijana wanaojiunga na JKT kwa mujibu wa sheria linafikiwa jeshi limendelea kujiimarisha kwenye mafunzo ya uzalendo,kuanzisha miradi ya uzalishaji mali pamoja na kuweka miundombinu rafiki.


Kwa upande wake mkuu wa kikosi cha 832 KJ Ruvu JKT Luten kanali CHARLES MBUNGE amesema katika kipindi cha miaka mitano iliyopita jeshi hilo limezidi kuboresha miundombinu ya kikosi hicho kwa kuongeza idadi ya mahanga ya kulala wanafunzi


Aidha jeshi hilo pia limejenga kituo cha mawasiliano ya mtandao ambacho kinawasaidia wanafunzi wanaojiunga na kikosi hicho kwa mujibu wa sheria kuweza kufuatilia matokeo yao ya kidato cha sita kiurahisi na pia kuomba nafasi za kujiunga na vyuo vya elimu ya juu wakiwa hapohapo jeshini.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company