Majibu ya James Mbatia kuhusu UKAWA kuzuiwa kutumia Uwanja wa Taifa na Kutoonekana kwa Dr. Slaa

James Mbatia ni mmoja wa Viongozi wa Umoja wa UKAWA, ambaye jana alikutana na Waandishi wa Habari kwenye Ofisi za Makao Makuu ya NCCR- Mageuzi, Ilala Dar

Miongoni mwa mambo aliyoyazungumzia ni UKAWA kuzuiwa kutumia Uwanja wa Taifa kwenye uzinduzi wa Kampeni zao, na kutoonekana kwa Dk. Slaa .

“Kampeni zinaanza nawasihi Wanasiasa wote wachunge ndimi zao sana, tujadili hoja kwa hoja kwenye majukwaa ya kisiasa sio kujadili watu, matusi, wala kupigana ngumi au kumwaga damu…

"Tume ya Uchaguzi ambayo ndio refa itende haki pamoja na vyombo vya dola… Wakitenda haki hakuna mgogoro wa aina yoyote, Kamati za Ulinzi na Usalama Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya hatutaki waingilie mchakato huu.“ alisema Mbatia

Kuhusu kuzuiwa Uwanja wa Taifa Dar, Mbatia alisema; “Uwanja wa Taifa ni mali ya Watanzania, tutakutana tutatafakari alafu tukishakubaliana kwa pamoja tutatoa taarifa wapi tutakutana na tutazungumza nini, kwa kweli hatuna majibu mpaka sasa hivi,"

Kuhusu swala la Dk. Slaa kutoonekana kwenye Vikao vya UKAWA, Mbatia alisema;

“UKAWA sio Mbatia, sio Slaa sio Lipumba sio Mbowe… tusijadili watu tujadili hoja za msingi za taifa, watu wanapita, tuzungumzie Watanzania zaidi“
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company