Mwandishi wa habari auwawa Sudan Kusini

Wanafamilia na raia wakitazama mwili wa mwandishi Peter Moi, nje ya nyumba ya kuhifadia maiti mjini Juba, Sudan Kusini, Agasti 20, 2015.
Mwandishi wa habari wa Sudan kusini amepigwa risasi hadi kufa, siku tatu baada ya rais Salva Kiir kutishia kuuwa waandishi ambao kwa maneno yake “ wako kinyume na nchi”

Mtu mwenye silaha alimuuwa Peter Moi aliyekuwa mfanyakazi wa gazeti la The New Nation newspaper jumatano jioni karibu na ofisi hizo mjini Juba. Wafanyakazi wenzake wanasema inaonekana kuwa alilengwa kwa sababu mshambuliani hakuchukua fedha za Moi wala simu yake ya mkononi.

Hakuna taarifa za awali kutoka kwenye jeshi la polisi au serikali. Waziri wa mambo ya nje wa marekani John Kerry alizungumza na bwana Kiir kwa njia ya simu ili kujadiliana kuhusu tukio hilo.

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imetoa wito kwa Juba kufanya uchunguzi wa kina kuhusu tukio hilo. Moi ni mwandishi wa habari wa saba kuuwawa sudan kusini mwaka huu. Jumapili rais Kiir aliwaambia waandishi wa habari huko Juba kwamba, “ kama kuna mtu kati yao hafahamu kwamba nchi hiyo imeuwa watu , tutaonesha siku moja, mara moja, na kwamba uhuru wa habari haumaanishi ni kufanya kazi kinyume cha nchi.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company