Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un akikagua jeshi lake wakati wa mafunzo ya kijeshi katika pwani ya mashariki ya peninsula ya Korea.
Reuters/路透社
Na RFI
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un amewaagiza wanajeshi wake kuwa tayari kuingia vitani kutokana na hali ya wasiwasi kati ya jeshi la nchi hiyo na lile la Korea Kusini.
Tangazo hili limetolewa baada ya kutokea kwa urushaji wa makombora katika mipaka ya nchi hizo mbili zinazoendelea kutishana mara kwa mara.
Vyombo vya habari nchini Korea Kaskazini zinaripoti kuwa uamuzi wa Kim Jong Un umefikiwa baada ya kikao cha dharaura na wakuu wa jeshi nchini humo.
Kiongozi huyo wa Pyongyang amewaambia wanajeshi kuwa tayari kuanza kutekeleza Operesheni na kuweka silaha zao tayari kuishambulia Korea Kusini na watasalia katika hali hiyo hadi kesho Jumamosi saa kumi na moja jioni.
Viongozi wa Jeshi nchini Korea Kusini wamemjibu kiongozi huyo wa Korea Kaskazini kwa kumwambia kuwa wako tayari kujilinda ikiwa watashambuliwa.
Tangu kumalizika kwa vita vilivyoigawa Korea mwaka 1953, mataifa haya mawili yameendelea kutishana kwa kushambuliana kijeshi hali inayoendelea kuzua hali ya wasiwasi katika Peninsula ya Korea.
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago