Waziri Mkuu wa Ugiriki ; Alexis Tsipras atangaza kujiuzulu

Alexis Tsipras anaonekana mdhaifu kutokana na kundi la zaidi ya wabunge arobaini kutoka Syriza.
REUTERS/Christian Hartmann
Na RFI
    Waziri Mkuu wa Ugiriki Alexis Tsipras ametangaza Alhamisi jioni kujiuzulu kwake ili kufungua njia kwa ajili ya uchaguzi wa haraka. Uchaguzi huo unaweza kufanyika tarehe 20 Septemba mwaka 2015.

" Katika muda mfupi, nitakwenda kwa Rais wa Jamhuri na kuwasilisha barua ya kujiuzulu kwangu na kujiuzulu kwa serikali yangu ", Alexis Tsipras ametangaza katika ujumbe alioutoa kwenye runinga Alhamisi jioni wiki hii. Waziri Mkuu ameongeza kwamba ametaka kuwasilisha kwa raia wa Ugiriki kila kitu alichofanya tangu kuchaguliwa kwake ili aamue upya. Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Ugiriki vikinukulu maafisa wa serikali, uchaguzi wa haraka ambao umeitishwa na Alexis Tsipras, unaweza kufanyika tarehe 20 Septemba mwaka 2015.

Alexis Tsipras hawakuwa na uamzi mwengine wa kuchukua. Anakabiliwa na mvutano uliozushwa na zaidi ya wabunge arobaini tangu kupitishwa kwa mpango wa tatu wa msaada kwa Ugiriki wa Euro bilioni 86 wiki iliyopita. Tawi hili la mrengo wa kushoto la Syriza limedhoofisha idadi kubwa ya wabunge alionayo, ambayo imepunguzwa wabunge 119 kwa jumla ya wabunge 300 wa Bunge la Ugiriki, na hivyo kuzuia sheria ya baadaye kuwasilishwa Bungeni.

Alexis Tsipras amelazimishwa kufuata utaratibu kwa kuwasilisha kwa rais Prokopis Pavlopoulos barua ya kujiuzulu kwa serikali na kuingia katika kampeni za uchaguzi kwa kipindi cha mwezi mmoja. Kaimu Waziri mkuu atakua kwa mara ya kwanza katika historia ya Ugiriki mwanamke, Vassiliki Thanou, mwenyekiti wa Mahakama ya kuu.

Hivyo raia wa Ugiriki watarejea kupiga kura kwa mara ya tano katika kipindi cha miaka sita.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company