PRO.LIPUMBA JIANDE KUITWA MSALITI

Salamu na pole kwa wote wanaoguswa na Mtikisiko wa hila katika Siasa ya TANZANIA,Jana niliaidi kuweka makala leo kuhusu kinacho endelea na kitakacho tokea kuhusu kujiengua katika UKAWA KW APRO. LIPUMBA Baada ya kujiuzulu uongozi kwenye chama chake cha CUF.

Sinadhumuni la kubariki wala kulaani alichokifanya Mwanaharakati na Jemedari huyu ila maamuzi haya kulingana na sababu zake yalichelewa na hakupaswa kumuunga mkono Lowassa kisha baadae kuja na kumkataa kwa madai ya dhamira kumuhukumu.

Ni kweli baada ya kosa ndipo dhamira hutoa hukumu ila alipaswa kutafakari na kuchukuwa mamuzi kam Dk.Slaa aliye susa mapema.

Kwani kumuunga mkono na kisha kutomuunga mkono jamii inaweza kubaki na maswali mengi na kujikuta wakitengeneza hoja nyingine hata kama ni dhaifu.

Jana alijitetea na kubainisha hivi;

“Nimejitahidi sana ndugu zangu kuvumilia, lakini dhamira inanisuta,” alisema Profesa Lipumba mbele ya waandishi wa habari jana kwenye Hoteli ya Peacock baada ya mkutano wa juzi aliopanga kufanyia ofisi za CUF kuzuiwa na wanachama.

“Sisi tumekaa tunaipigia kelele Rasimu ya Katiba ya (Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyokuwa chini ya Jaji Joseph) Warioba lakini iliyopitishwa ni Katiba Inayopendekezwa sasa tunawachukua waliopitisha ili waje kuisimamia. Hivi inaingia akilini?”

Ok, ila rai yangu siku ya leo kwa Pro. Lipumba ajiandae kuitwa msaliti tena mzushi kutokana na maamuzi aliyoyachukuwa,jambo hili ni la kawaida katika siasa changa na dhaifu kama za nchi yetu kwani ili uonekane ni shupavu ni lazima ukubaliane na matakwa yote ya upinzani na usipofanya hivyo unahesabiwa kama msaliti na kibaraka wa CCM.

Jambo hili halitakuwa geni kwako kwani hata kwa Zito ndicho kilichofanyika wakati swala lilikuwa ni kutofautiana katika hoja.

Kila la heri na ninakutakia mafanikio mema ila wito wangu Kwa wanaukawa nikutafakari kwa kina kilichotokea naniungane na Mtatiro kuwataka watanzania kutokumtukana wala kumlaumu kwani alikuwa ni shujaa ama kamanda wamsari wa mbele aliyefia vitani.

Ukawa bado nafasi yakutengeneza ipo wala msidhubutu kupanda adharani kumtuka amtolea maneno ya ashifa huyu jemedari kwani haitaingai akilini pale mtakapo muita msaliti amaantumika na CCM eti kwa kujiondoa Kwenye uongozi wakati toka wali alipamban ana hadi sasa ankesi kwa Mahakamani kwa ajiliyakukitetea chma na mara nyingi aalikuw tayari kuhatarisha maisha yake pamoja na muda wake kwa ajili ya mapambano ya ukombozi.

UKAWA ZIBENI UFA NA MKUBALI MAKOSA.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company