Rais Kikwete, alilazimika kwenda na Zitto Kabwe nchi za Mashariki ya mbali kusaka misaada ya ujenzi wa barabara za Mkoa wa Kigoma na Daraja la Malagarasi kutokana na kelele zake bungeni.
Kwa ufupi
Asema alimshirikisha kwenye safari zake za nje kwenda kuomba misaadaBy Anthony Kayanda, Mwananchi
Kigoma. Rais Jakaya Kikwete amesema alilazimika kufuatana na aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini wa Chadema kwa wakati huo, Zitto Kabwe kwenda nchi za Mashariki ya mbali, kuomba misaada ya ujenzi wa barabara za Mkoa wa Kigoma na Daraja la Mto Malagarasi ili kuunganisha na Mkoa wa Tabora.
Akihutubia wakazi wa Kigoma wakati wa ziara yake ya siku mbili mkoani hapa juzi, Rais Kikwete, alisema alilazimika kufanya hivyo kutokana na kelele za Zitto ndani ya Bunge la Tisa la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.|
Alisema aliamua kumshirikisha Zitto ambaye kwa sasa ni Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo kwenye safari yake ya kwanza kwa nchi hizo za Japan, China na Korea Kusini.
Alifafanua kuwa alifuatana na Zitto ili awe shahidi kwa jinsi alivyokuwa akisafiri kwenda kwenye nchi hizo kuomba misaada.
Kikwete alisema pia, alitumia fursa hiyo kumuomba Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Ban Ki Moon, wakati huo akiwa Waziri wa Nje wa Korea Kusini ili kuhakikisha nchi hiyo inatoa fedha za kujenga daraja hilo.
“Nilipokuwa Kigoma mwaka 2005 kuomba udhamini ndani ya CCM na hata nilipokuwa kwenye kampeni za uchaguzi mkuu, niliambiwa mojawapo ya changamoto kubwa za Kigoma ni ukosefu wa barabara za lami kuunganishwa na mikoa mingine, pia kukosa daraja Mto Malagarasi ili kuiunganisha Kigoma na Tabora,” alisema Kikwete na kuongeza kuwa:
“Kuhusu Daraja la Malagarasi, nilianza harakati za kulijenga nikiwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa kuomba msaada kutoka Korea Kusini. Nafurahi kwamba kipindi changu cha miaka 10 ya urais kinamalizika ujenzi wa daraja umekamilika, barabara karibu zote zimejengwa na hata zile ambazo hazijakamilika ninaamini akipita (John) Magufuli kuwa Rais atazimalizia.”
Aliwataka wakazi wa Kigoma kuendelea kuwa wavumilivu kutokana na kukwama kwa ujenzi wa mradi wa maji ya bomba kwa ufadhili wa Jumuiya ya Nchi za Ulaya (EU), uliotakiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi huu baada ya mkandarasi kukumbwa na matatizo binafsi.
#USOPEN_VIGOGO CHALI
-
SIKU Safi kwa Muaustralia Nick Kyrgios baada ya ushindi dhidi Johnson na
kutinga raundi ya Pili.
- Rafael Nadal akimchapa Millman Seti Tatu zote mfululi...
5 years ago