Joto Lazidi Kupanda....UKAWA Wafungua Kesi Mahakamani Kupinga Wananchi Kuzuiwa Kulinda Kura

Leo tarehe 16 October 2015, Ukawa kupitia wakili wa CHADEMA,Peter Kibatala na mawakili wengine, wamefungua chini ya hati ya haraka sana (certificate of extreme urgency) shauri nambari 37 la mwaka 2015 katika Mahakama Kuu ya Tanzania (Main Registry) wakiomba Mahakama Kuu itoe tafsiri sahihi ya kifungu cha 104 (1) cha Sheria ya Uchaguzi Tanzania na itamke iwapo wapiga kura na watu wengine wenye shauku wanaruhusiwa au la kukaa KWA UTULIVU umbali unaozidi meter 200 kutoka kituo cha kupigia kura/kufanya majumuisho ya kura.

Pia wameiomba Mahakama Kuu itamke iwapo ni halali kwa Rais wa nchi kutoa matamko aliyoyatoa kwa namna ya katazo kwa wapiga kura/raia wenye shauku kukaa KWA UTULIVU umbali unaozidi mita 200 kutoka kituo cha kupigia kura/kufanya majumuisho.

Pia wameiomba Mahakama Kuu itamke iwapo Rais ana mamlaka hayo kisheria kwa kuzingatia Sheria ya Uchaguzi Tanzania.

Taarifa hii ni kwa mujibu wa Wakili Peter Kibatala ambaye ameshare nasi kwenye ukurasa wake wa facebook

Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company