HABARI KUU ZA LEO na OSCAR SAMBA
print this page
HABARI NA Oscar Samba
Showing posts with label MICHEZO/BURUDANI. Show all posts
Showing posts with label MICHEZO/BURUDANI. Show all posts

Arsenal watingwa magoli matano na Bayern

Arsenal watahitaji kushinda mechi zilizosalia na waombe sana Olympiakos washindwe mechi zilizobaki
Arsenal wanakabiliwa na kibarua kigumu katika juhudi zao za kutaka kufuzu kwa hatua ya muondoano Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya baada ya kupokezwa kichapo kikubwa na Bayern Munich.

Mambo yalianza kuenda mrama upande wa The Gunners kipindi cha kwanza baada ya bao la kichwa kutoka kwa Robert Lewandowski (dakika ya 10), na makombora kutoka kwa Thomas Muller (Dakika ya 29) na David Alaba (Dakika ya 44)kuwaweka wenyeji 3-0 mbele kufikia muda wa mapumziko.

Arjen Robben kisha alifunga bao dakika ya 55 kipindi cha pili na ingawa Olivier Giroud alifungia Arsenal bao la kufutia machozi dakika ya 69, Muller aliongeza bao jingine dakika ya 89 na kukamilisha kichapo hicho.

Kushindwa huko kwa Arsenal Ulaya, ambako kunafikia rekodi ya kichapo kibaya zaidi kupokezwa timu hiyo barani humo, kinawaacha Arsenal wakiwa alama sita nyuma ya Bayern na Olympiakos zikiwa zimesalia mechi mebili pekee.

Ushindi wa 2-1 wa klabu hiyo ya Ugiriki dhidi ya Dinamo Zagreb unamaanisha kwamba sasa Arsenal hawana usemi kuhusu uwezekano wao wa kufuzu na wamo hatarini ya kushindwa kufika hatua ya muondoano kwa mara ya kwanza katika misimu 13.

Arsenal walikuwa wamepata matumaini majuma mawili yaliyopita walipochapa Bayern 2-0 uwanjani Emirates lakini sasa hayo yote yamefutika.Cech aliokoa mipira muhimu lakini hakuweza kuokoa Arsenal

Sasa lazima wafute pengo la alama sita kati yao na Olympiakos, ambao watakutana nao Desemba 9 baada ya kukutana na Zagreb Novemba 24.

Arsenal wanahitaji kuchapa Zagreb na waombe sana Olympiakos washindwe mechi yao ijayo ugenini kwa Bayern, ambao bado pia hawajafuzu kwa hatua ya muondoano.

Hilo litaacha Arsenal na ‘fainali’ ya kufa kupona nchini Ugiriki ambako Gunners watahitajika kulaza Olympiakos kwa mabao mawili ya wazi, ikizingatiwa kwamba walichapwa 3-2 na klabu hiyo uwanjani Emirates Septemba 29.

Takwimu muhimu
Kichapo hicho kinatoshana na kichapo kikubwa zaidi walichowahi kupokeza Arsenal Ulaya, waliposhindwa 4-0 na Milan Februari 2012.
Arsenal wamefungwa mabao matano Ulaya kwa mara ya pili sasa (5-2 v Spartak Moscow katika Kombe la Uefa 1982/83).
Lewandowski amefunga mabao saba katika mechi zake saba alizocheza Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya
Robben alifunga baada yake kuwa uwanjani sekunde 37 pekee (ilikuwa mara yake ya kwanza kugusa mpira)
Giroud amefunga bao katika mechi tatu kati ya nne walizocheza Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Bayern Munich.

Twaelekea wapi sasa?

Arsenal watakaribisha nyumbani Tottenham Jumapili nao viongozi wa Bundesliga Bayern wawe nyumbani dhidi ya Stuttgart Jumamosi.
0 Toa maoni yako.

Diamond Na Mpenzi Wake Zari Wapata Mtoto Wa Kike.

Staa wa Bongo Fleva ambaye jina lake limebeba uzito mkubwa Afrika,Diamond Platnumz amepata mtoto wa kike toka kwa mpenzi wake Zari Hassani.

Mtoto huyo ameingia duniani saa 10 na dakika 40 Alfajir, Alhamis hii.

Haijaweza kufahamika kwa mara moja ni hospitali gani mtoto huyo amezaliwa kwa kile meneja alichosema ‘usalama wa mama na mtoto’ kwakuwa bado wapo hospitali.

“Sura ya mama yangu inatosha kueleza ni kiasi gani najiskia ndani ya Moyo wangu, karibu kwenye ulimwengu @princess_tiffah,” ameandika Diamond kwenye picha hiyo juu aliyoiweka Instagram.

Awali Diamond alisema kuwa Zari angejifungulia Tanzania.
0 Toa maoni yako.

Lembeli ashinda kura za maoni Chadema, Bulaya almanusura.......Viti maalumu vyamuokoa

Wabunge wawili waliohama CCM hivi karibuni, James Lembeli na Ester Bulaya wamepitishwa katika kura za maoni kuwania ubunge kupitia chama chao kipya.

Wakati Lembeli akipitishwa kwa kura za kishindo kuwania ubunge katika Jimbo la Kahama Mjini, Bulaya alishinda katika nafasi ya viti maalumu baada ya kushindwa katika kinyang’anyiro cha Jimbo la Bunda Mjini.

Wanasiasa hao sasa wanasubiri uteuzi wa Kamati Kuu ya Chadema utakaofanyika Agosti 5 na 6.

Ushindi wa Lembeli
Katika uchaguzi huo wa juzi, mbunge huyo wa zamani wa Kahama aliwabwaga wenzake 13 aliogombea nao akipata kura 168 kati ya 262 zilizopigwa, akifuatiwa na John Katibu aliyepata kura 45, Peter Shita (17) na Emmanuel Madoshi aliyepata kura 10.

Wengine ni Muta Nyerere (4), Felician Maige (4), Zacharia Obadia (3), Tadeo Mwati (2), Arnold Mtajwaka (2), Prosper Denga (2), Deusdedit Madinda (1), Reuben Macheyeki (1). Victor Mbwana na Richard Makingi waliambulia patupu. Katika uchaguzi wa viti maalumu, Winfrida Mwinula alishinda kwa kura 34 akifuatiwa na Salome Makamba aliyepata kura 30.

Bulaya
Kama isingekuwa ni kura za maoni za viti maalumu zilizomfuta machozi, Bulaya alikuwa tayari ametupwa nje baada ya kuanguka katika Jimbo la Bunda Mjini.

Bulaya aliyekuwa miongoni mwa makada saba wa chama hicho waliokuwa wanawania kuliwakilisha jimbo hilo, alipata kura 37 kati ya 182 zilizopigwa akiwa nyuma ya Pius Masururi aliyeibuka mshindi kwa kura 65 na Magembe Makoye aliyepata kura 40.

Baadaye katika mkutano wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha), uliofanyika baadaye usiku, Bulaya alipata kura 71 kati ya 110 zilizopigwa na kuwabwaga Godliver Masamaki aliyepata kura 31, Joyce Sokombi (4), Minza Shani (3), Dk Jane Nyamsenda (1) na Alice Wandya aliyeambulia patupu.

Awali, Bulaya alikwaa kisiki baada ya jina lake kuwa miongoni mwa waliokatwa na kamati ya utendaji inayosimamia majimbo hayo wakidaiwa ni wageni katika chama; wapenda fujo na matabaka, akiwa pamoja na Chacha Nyamhanga, Sulemani Daudi lakini walirudishwa kundini baada ya kikao cha viongozi na watiania.

Katika Jimbo la Bunda Vijijini, Sulemani Daudi aliibuka mshindi kwa kura 84 kati ya 127 zilizopigwana kuwashinda John Masenza aliyepata kura 14, Dk Lucas Webiro (11), Frank Mongateko (8), Edgar Chibura (5) na Mathias Bandio aliyepata kura moja.
0 Toa maoni yako.

BASATA imemfungia Shilole Mwaka Mmoja, Hakuna Kufanya Muziki

Baraza la sanaa Tanzania (BASATA) limemfungia mwanamuziki Zuwena Mohamed ‘Shilole” kutojihusisha na kazi yoyote ya sanaa kwa muda wa mwaka mmoja kutokana na kukiuka sheria na maadili.

Barua ya BASATA imesomeka hivi “Tarehe 9 May 2015 ukiwa katika onyesho lako la muziki Ubelgiji ulicheza uchi mbele ya hadhira ya wapenda sanaa za Tanzania hivyo kudhalilisha utu wako na jamii ya kitanzania kimaadili”.


“BASATA ilipata habari zako, kumbuka pia October 2013 BASATA lilikuonya na ukakiri kwa kuomba msamaha tabia yako ya kucheza bila kuzingatia maadili uwapo jukwaani, BASATA ilikupa nafasi ya kutoa maelezo kwanini usichukuliwe hatua za kinidhamu kwa kitendo chako lakini umekaidi kutoa maelezo yako”.


"Baraza limejiridhisha kwamba ulikiuka maadili ya kazi ya sanaa kwenye onyesho lako huko Ubelgiji makusudi na umekiuka sheria kwenye ibara ya 30 (2) ya katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 kwa kuvunja maadili ya jamii ya Mtanzania hivyo baraza linakusimamisha kujishughulisha na kazi za sanaa nchini na nje ya nchi kwa mwaka mmoja, kufanya kinyume na hayo kutapelekea kupewa adhabu zaidi pamoja na yeyote utakaeshirikiana nae”.
0 Toa maoni yako.

Msanii Hafsa Kazinja aokoka baada ya kukutana na mauzauza jukwaani

MWANAMUZIKI aliyeamua kumgeukia Mungu na kuokoka, Hafsa Kazinja aamebainisha kuwa alikuwa akiteswa na mauzauza ya kishirikina pindi alipokuwa katika majukwaa akiimba Bongo Fleva.

 Hafsa alisema alikumbana na mambo mengi sana ya ajabu ikiwemo kuona majoka makubwa jukwaani akiwa anatumbuiza na sauti za ajabu za mara kwa mara.

“Nilikuwa naishi maisha ya ajabu sana jamani yaani, nikiwa jukwaani naimba basi naanza kusikia sauti za ajabu mara naona majoka makubwa yanapita pita mbele yangu na kunifanya niishiwe pozi katika utumbuizaji wangu, hayo yote najua zilikuwa chuki za binadamu, nashukuru tangu niokoke hivi sasa sina matatizo hayo kabisa,” alisema Hafsa
0 Toa maoni yako.
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company