Friday Feb 22, 2013
Login |
Usaili
| Text Size
[-]
[+]
<a
href='http://www.ripoti.com/openx/www/delivery/ck.php?n=a5831c86&amp;cb=INSERT_RANDOM_NUMBER_HERE'
target='_blank'><img
src='http://www.ripoti.com/openx/www/delivery/avw.php?zoneid=387&amp;cb=INSERT_RANDOM_NUMBER_HERE&amp;n=a5831c86'
border='0' alt='' /></a>

Mwenyekiti Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii, Magreth Sitta
Mwenyekiti wake, Magreth Sitta alitoa wito huo juzi baada ya kamati
yake kutembelea mpaka wa Tanzania na Malawi katika eneo la Kasumulo
wilayani Kyela na Mto Songwe unaotenganisha nchi hizo kwa umbali wa
zaidi ya kilometa 15.
Akiwa katika maeneo hayo, alishuhudia njia nyingi za panya
zinazotumika kuingiza nchini bidhaa za vyakula kama vile sukari na
vipodozi ambavyo baadhi yake havijasajiliwa nchini.
Alisema kuna baadhi ya dawa na vipodozi ambavyo havikubaliki
nchini lakini katika baadhi ya nchi za Sadc vinakubalika hali ambayo
inasababisha udhibiti wake kuwa mugumu.
Alisema ili kuondokana na hali hiyo ni vema sheria za Tanzania
zikaoanishwa na zile za nchi za Sadc ili bidhaa za aina moja ziruhusiwe
kutumika kwenye nchi zote za Jumuiya hiyo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kyela
ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Magreth Ester Malenga alisema kuwapo
kwa bidhaa ambazo hazikubaliki nchini lakini zinatumika katika nchi
jirani kunatoa changamoto kubwa kwenye ulinzi wa mipaka hasa katika
kudhibiti zisiingizwe nchini kwa magendo.
Alisema kwa sasa sheria ya Tanzania hairuhusu kuingizwa kwa sukari
kutoka Malawi, lakini wakati huo huo kuna uhaba mkubwa wa bidhaa hiyo
wilayani humo, hali ambayo inatoa changamoto kubwa kwake binafsi kama
Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya na kwa vyombo vya
dola.
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid, alisema
Serikali itaufanyia kazi ushauri uliotolewa na Kamati hiyo, hasa ule
ambao uko chini ya wizara yake na kuihakikishia kuwa suala la
ushirikiano baina ya Tanzania na nchi jirani litaimarishwa
CHANZO:
NIPASH

