Muungano wa Ulaya umeahidi kuipa
Somalia dola milioni 862 kama msaada. Ahadi hii imetolewa kwenye
kongamano la kimataifa lililoandaliwa mjini Brussels Ubelgiji,
kutathmini maendeleo yaliyofikiwa nchini Somalia, tangu vitra kupungua.
Pesa hizo zitatumika kufadhili miradi ya kuikarabati Somalia ambayo imekumbwa na vita kwa miongo miwili.Mkutano huo unawaleta pamoja maafisa wa serikali , mashirika ya misaada na taasisi za kifedha.
Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud, aliambia BBC kuwa mkataba mpya unaopendekezwa na ambao unaipa nchi hiyo usemi mkubwa kuhusu mahitaji yake ya maendeleo, utaifaidi nchi ya Somalia pakubwa sana.
Duru zinasema kuwa matatizo chungu nzima yangali yanaikumba Somalia ikiwemo serikali kudhibiti sehemu ndogo tu ya nchi na ripoti za utumizi mbaya wa pesa.