Na Oscar Samba
Siku chache zilizo pita mji wa Arusha uliibua hisia zankutisha kutokana na majanga mawili ya mlipoko wa mabomu yaliyotokea kwa nyakati na sehemu mbili tofauti.
La kwanza lilikuwa ni mlipuko wa bomu kanisani na la pili kwenye mkutano wa chama cha CHADEMA,malaki kwa mamilioni ya watanzania pamoja na watu kutoka kona mbalimbali za dunia wali laani vitendo vile.Matukio hayo yalitwa uhai wa watu zaidi ya saba huku makumi wakijeruliwa,lakini lipo janga jingine lililo kidhiri sana ambalo hutwaa uhai wa watoto wadogo kila uchwao cha ajabu mashirika ya kimataifa,serikali na wanaharakati hawalipi kipaumbele.
Wakati huu nikiwa ninaandika makala hii kichwa changu kinauma kutokana na taarifa nilizo zipata za utoaji mimba kutoka kwa mwanafunzi mwenzangu,sii yeye tuu bali matukio kama haya katika yvuo mbali mbali ya mekithiri, najua sii wanafunzi pekee ila rekodi zangu za kiuchunguzi zimewanasa wanafunzi zaidi.
Kuna binti mmoja hadi sasa anajigamba ya kwamba kaashatoa mimba zaidi ya nne ikiwemoaliyoitoa siku chache,bila aibu hutaja hadi hosipitali na kiasi cha fedha.
“Nilitumiwa elufu sabini na baba ya kula nikaenda pale nikawapa elufu hamsini” alinena binti huyo ambae jina nimemuifadhi kwa sasa na nikikamilisha uchunguzi wote nitawaweka adharani pamoja na hosipilali sugu hapa nchini.
Mwaka jana nikiwa katika visiwa vya Zanzibar eneo la Forodhani majira ya jioni nilimsikia dakitari mmoja akielezea ya kwamba yupo mama mmoja alitaka kutoa mimba cha ajabu ameolewa na ana watoto wengine ,daktari yule alimkubalia lakini alimpa shariti mmoja lililomtaka aje na mwanae siku ya tukio,siku ilipo mdia alifanya hivyo.
Dakitari alitaka kujua sababu za yeye kufanya hivyo nae alidai ya kwamba mtoto aliopo ni mdogo mno na mimba aliyoipata ilikuwa ni bahati mbaya,dakitari alimtwaa mtoto aliekuja nae kisha akamwambia mama waanze kumuua mtoto yule,kwa hofu mama alipiga kelele.Ndipo dakitari alipomwambia ya kwamba mimba aliyo nayo pia imebeba mtoto na wote dhamani yao ni sawa,mama yule aliondoka na hakutoa tena mimbna ile.
Pia dakitari yule alisimulia uasi anaoufanya dakitari mwenzake ambae kutoa mimba kwake sii jambo la kushangaza,yeye anashariti moja kuu kabla ajamtoa msichana/mwanamke mimba ni lazima akubali kujamiianae kwanza akikataa na zoezi halifanyiki na wengi hukubali,niliguswa zaidi na ushuhuda huu,dakitari alisema kwamba iposiku mmoja alikuja msicha na mpenzi wake walikuwa bado hawajaoana dakitari yule dhalimu akawaita pembeni na kuwapa shariti lile kijana yule wakiume aliposikia hivyo alitaamaki na kuamua waondoke,siku chache walirejea tena kwa unyenyekevu na bila aibu mvulana yule alikubali mwenzake yaani yule dakitari dhalimu ajamiiane na mpenzi wake eti kisa ili akubali kufanya mauaji.
Huwo ni uzalilishaji waaina gani,visa ni vingi tena vyakutisha,matukio haya ya utoaji mimba hutokea katika kona mbalimbali za nchi yetu bila kubagua visiwani au bara mijini wala vijijini na wanaofanya hivi sii wasioojua madhara yake tuu bali hata wasomi.
Sababu kubwa ya matendo haya ya utoaji mimba siioni kwani ni nani aliempa mwanadamu uhalali na mamlaka ya kufanya machafu hayo, ni katiba ya nchi yetu ? laa asha!!, vitabu vya dini? Jibu ni hapana,mila na desturi zetu? Au maadili ya ukunga na udakitari ?Hakika hakuna majibu ya ndio.
Kama ndivyo tunapata wapi ujasiri wa kufanya mabaya hayo? Embu swali tujiulize kama mzazi wako na wangu angali fanya uwasi kama huo tungali kwepo duniani siku ya leo? Kama jibu ni siyo kwa nini mimi na wewe kwanzia sasa tusiwe majemedari,makamanda na maasikari pia sungusungu watakao ongoza vita hivi vya kupinga utoaji wa mimba?
Narudia tena mimi binafsi naamini ya kwanmba hakuna sababu ya kijamii wala kiuchumi inayoweza kumfanya mtu atoe mimba, labla zile za kitabiba (za kiafya)
Kwa mujibu wa uchunguzi mdogo nilioufanya baadhi wanajitetea ya kwamba eti umasikini ni sababu,mama yeye anaweza kuishi mtoto atashindwa nini,wengine wanaume kukataa mimba; nayo hii hainiingi akilini kwani mzazi mmoja huweza kumlea mtoto,mfano kuna waziri mmoja hapa nchini tunaemsifia sana ya kwamba ni mchapa kazi mama yake alitaka kutoa mimba yake kwani baba yake aliikana na kukataa kumuoa,ila alijipa moyo baada ya mateso ya manyanyaso na shida nyingi akabaatika akaolewa na mtu mwingine alikubali kumlea mtoto yule,leo ni waziri anaelisaidia Taifa la Tanzania hadi kufikia hatua ya kuitwa mchapa kazi.
Wapo wanaosema ya kwamba tukio la kubakwa,kwa sauti ya ujasiri na yenye kujiamini na sema sababu hii ni dhaifu ingawajke wachache huitetea,leo hii Ophara Wilfred ni miongoni mwa wanawake waliopo kwenye kumi bora ya matajiri wa nchi ya Marekani lakini dada huyu aliwahi kubakwa na baba yake mzazi baada ya kuugua ugonjwa wa akili; hakuamua kuitoa mimba aliyoipata aliilea na hatimae kujifungua.
Wala hamuonei aibu mtoto aliyezaliwa,nchini Marekani kuna muubiri mkubwa wa injili ambae mama yake alibakwa ndipo yeye akazaliwa,leo amefanyika msaada kwa wengi.
Ni kweli ya kwamba wapo wazazi wengine ambao ni wakali kwa watoto wao hususani anapokuwa chuo/shuleni kisha wakagundua ya kwamba ni mjamzito, ila sababu hii isikufanye ufanye dhambi ya mauaji; kuliko uuwe ni bora ukakubali mateso na matukano yote ila uchunge uhai wa kiumbe ulichopewa na Mwenyezi Mungu.
Kuna binti mmoja anaitwa Aisha nimesoma nae ngazi ya cheti cha juu,mara tu alipopata ujauzito wazazi wake walimtaka atoe lakini alikataa leo mtoto wake anatembea na wazazi wake wanampenda mjukuu wao kuliko hata mama yake,kwa kuwa damu ni nzito kuliko maji naamini wazazi hawatakutupa bali kelele na matukio ya tokanayo na hasira lazima vita kwepo.
Wito wangu kwa jamii na serikali, hili janga la utoaji mimba na utupaji wa watoto wachanga lifanywe la kitaifa; na vita hivi vipangiwe mikakati kama ilivyo vita dhidi ya dawa haramu za kulevye,maleria na unyanyasaji wa kijinsia.Kwani mauaji ndio janga kubwa kupita yote, pia madakitari na wauguzi zingatieni maadili yenu ya kazi acheni tamaa,wazazi na walezi punde tatizo litokeapo watoto wenu msii wajengee mazingira yatakayo wapelekea kufanya vitendo kama hivyo.
Enyi wanaume/wavulana na wazazi mnaoshindikiza na kuwezesha ushenzi huu acheni mara moja, pia serikali/yapaswa kufanya tafiti ilikuwabaini wahusika na kuwachukulia hatua kali, elimu pia haina budi kutolewa mashuleni na majumbani, mimi na wewe tukiamua tunaweza kutokomeza udhalimu howo.
Tafadhali kwa maoni wasiliana nami,simu;0759859287 au barua pepe; hakileotanzania@gmail.com ama tembea bloguhii; www.hakileo.blogspot.com.